Raia wa Niger wakiandamana kupinga uwepo wa jeshi la marekani, Agadez / Picha: Reuters

Mamia ya watu waliandamana Jumapili wakipinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Niger ambako ujumbe kutoka Washington unatarajiwa kuwasili ndani ya siku chache kupanga utaratibu wa kuondoka.

Mnamo Ijumaa, Marekani ilikubali kuwaondoa zaidi ya wanajeshi wake 1,000 walioko taifa hilo la Afrika Magharibi ambako Washington ilijenga kambi ya dola milioni 100 kwa ajili ya kuendesha ndege zisizokuwa na rubani.

Maandamano hayo katika mji wa jangwa la Kaskazini mwa Agadez, iliyoko kambi hiyo inayotumika kama ngome kuu ya mashambulio ya anga ya Marekani, yaliandaliwa na makundi 24 ya asasi za kiraia ambazo zimeunga mkono utawala tangu mapinduzi ya mwaka jana.

"Hapa ni Agadez, sio Washington, jeshi la Marekani lirudi nyumbani," ilisoma bango kubwa lililoshikiliwa na waandamanaji.

Issouf Emoud, kiongozi wa Harakati ya M62 mjini humo, aliliambia shirika la habari la AFP, "Ujumbe wetu uko wazi: wanajeshi wa Marekani wapakie mifuko yao na kwenda nyumbani".

Kwa muda mrefu, Niger imekuwa mhusika muhimu katika mkakati wa Marekani na Kifaransa wa kupambana na makundi ya kigaidi katika Afrika magharibi.

Mwezi uliopita, jeshi la Niger lilitangaza kuwa litavunja makubaliano ya ulinzi na Marekani, likidai kuwa liliwekwa kwa lazima na uwepo wa wanajeshi wa Marekani ulikuwa kinyume cha sheria.

Kufuatia kupinduliwa kwa rais aliyechaguliwa Mohamed Bazoum Julai iliyopita, junta ilifukuza wanajeshi kutoka kwa kolono hiyo ya zamani ya Ufaransa kabla ya mwisho wa 2023.

AFP