Waziri wa uchukuzi nchini Kenya Kipchumba Murkomen amefanya mabadiliko katika usimamizi wa viwanja vya ndege Jumamosi, baada ya mashauriano na bodi ya usimamizi.
Shirka hilo la viwanja vya ndege KAA limekumbwa na shutuma baada ya kuathiirka na kukatika kwa umeme nchini ambapo kiwanja kikubwa cha usafiri wa ndege Kenya JKIA kiliathirika.
Awali waziri Murkomen alinukuliwa kusema kuwa KAA imekabiliwa na msururu wa makosa yaliyosababishwa na changamoto za usimamizi na uingiliaji wa kisiasa ambao umesababisha wafanyakazi kuvunjika moyo na kutowajibika kazini.
''Bodi imefanya kazi kubwa katika uundaji upya na ukarabati wa KAA.'' Alisema waziri Murkomen. ''Taasisi hiyo imeanza mchakato wa kuajiri watumishi wa kudumu kuchukua nafasi hizi, katika zoezi litakalohitimishwa ndani ya wiki mbili zijazo.'' aliongeza Waziri.
Uteuzi na Utenguzi
Bw. Alex Gitari ambaye amekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya amesimamishwa kazi. Katika nafasi yake, Bw. Henry Ogoye ambaye kwa sasa anahudumu kama mratibu wa mipango ya mashirika ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KAA.
Fred Odawo ambaye amekuwa Meneja Mkuu, huduma za mradi na uhandisi ametenguliwa, na badala yake Mhandisi Samuel Mwochache ameteuliwa katika nafasi ya kukaimu.
Abel Gogo, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa JKIA sasa anahamia
Selina Gor, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu sasa
Peter Wafula, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mombasa anahamia
Safari ziko salama
Katika taarifa yake, waziri Murkomen aliwahakikishia Wakenya kuwa safari hazikukatizwa Ijumaa wakati umeme uwanja huo uliathirika na kukatika kwa umeme sehemu nyingi nchini.
''Ningependa kuomba msamaha wa dhati kwa wasafiri wote na watumiaji wa uwanja wa ndege ambao waliathiriwa kwa njia moja au nyingine na kukatika kwa umeme huko JKIA,'' alisema waziri Murkomen.
''Ili kuepusha mashaka, tukio hilo ingawa la kusikitisha halikusababisha hatari yoyote kwa safari za ndege za abiria zinazoingia na kutoka kwa kuzingatia kwamba jenereta chelezo huwasha njia ya kurukia ndege na kudhibiti mnara,'' aliongeza.
Waziri Murkomen amekuwa katika mkutano wa dharura na wasimamizi na wadau wa safari za ndege jijini Nairobi kuanzia asubuhi Jumamosi ambapo ametoa hakikisho kuwa shughuli zimerejelewa kawaida katika viwanjza vya ndege.