Maelfu ya watu walifariki kufuatia janga la hivi karibuni la mafuriko nchini Libya / Picha: AA

Taarifa kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu ilisema kuwa maafisa hao, wakiwemo waliohudumu awali na sasa katika ofisi zinazohusika na idara ya maji na usimamizi wa bwawa, wanashukiwa kuhusika na "usimamizi mbovu" na uzembe.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Libya Al-Seddik Al-Sur amesema kuwa baada ya uchunguzi kufanyika kwa zaidi ya wiki moja iliyopita, mabwawa mawili yaliyo juu ya Mto kutoka Derna yalikuwa yamepasuka tangu mwaka1998.

Hata hivyo, marekebisho yaliyoanzishwa na kampuni ya Uturuki mnamo 2010 yalisitishwa bila kuanza tena kufuatia mapinduzi ya Libya ya 2011, mwendesha mashtaka alisema mnamo Septemba 16, huku akiapa kuwachukuliwa hatua waliohusika.

Tangu mapinduzi hayo ya Libya ya 2011, bajeti ilikuwa inatengwa kila mwaka kukarabati mabwawa hayo mawili, lakini hakuna serikali yoyote iliwahi kufanya kazi hiyo, hayo ni kulingana na afisa hiyo.

Mabwawa yote mawili yalijengwa na kampuni ya Yugoslavia miaka ya 1970, "Sio kukusanya maji lakini kulinda Derna kutokana na mafuriko," Sour alisema awali.

Kufikia siku ya Jumamosi, idadi rasmi ya vifo ilifikia watu 3,800, huku vikundi vya misaada vya kimataifa vikisema kuwa huenda watu 10,000 au zaidi wakakosekana baada ya mafuriko ya ghafla, ambayo mashahidi walifananisha na tsunami.

Mabwawa hayo mawili makongwe yalipasuka mnamo Septemba 10 baada ya dhoruba kali ya kimbunga kugonga eneo la karibu na Derna, mji wa bandari mashariki mwa Libya.

AFP