Na Mazhun Idris
Kati ya mambo yaliyotawala ziara ya hivi karibuni ya mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan, nchini ni Nigeria ilikuwa ni onesho la michoro yaliyoandaliwa na msanii wa kutoka taasisi ya Yunus Emre, ikionesha baadhi za kazi za wasanii wanawake kutoka Afrika Mashariki.
Kati ya wasanii walionogesha maonesho hayo ni pamoja na Halima Abubakar, ambaye kazi zake zenye tamaduni mseto, zilimfurahisha mke wa Rais wa Uturuki.
"Sanaa yangu huhusisha Mandala, Tezhip and Dotilism," Halima anaiambia TRT Afrika.
Tezhip ni neno la Kituruki linalomaanisha "kupamba kwa dhahabu". Katika kipindi cha Ottoman, ilikuwa mila ya ubunifu ya kupamba mapambo ya maandishi kwa kutumia wino, hati na michoro mbalimbali.
Katika misikiti na vituo vingine vya kidini, kazi za Tezhip zimetawala nyota ndani ya majengo hayo, zikiwakilisha tamaduni za Mashariki ya Kati.
Kwa upande mwingine, ni aina ya sanaa inayotumia miundo na mifumo ya kijiometri, ambayo awali inaashiria ulimwengu katika Uhindu na Ubuddha.
Sanaa ya vidoti huhusisha uwekaji vitone vingi kwenye uso ili kuunda umbile na kina kabla ya kutumia rangi.
Uwekaji wa vidoti hivyo hufuata mwingiliano linganifu wa rangi ili kuwiiana katika rangi.
Kazi aipendayo
Safari ya ubunifu ya Halima ilianza muongo mmoja uliopita alipojianika na sanaa ya Mandala kwenye Instagram. Alikuwa na umri wa miaka 18 wakati huo na mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Bayero huko Kano, kaskazini-magharibi mwa Nigeria, ambako alihitimu katika biokemia.
"Niliwasiliana na wataalamu wa Dubai na India, miongoni mwa nchi nyingine za Asia, kwa ufahamu wao kuhusu aina hii ya sanaa ambayo niliipata ya kuvutia sana. Lakini hakukuwa na jibu kutoka kwa yeyote kati yao," anasema Halima, akikumbuka juu ya msukumo wake.
Aliwatafuta wasanii wa Mandala nchini Nigeria ambao wangeweza kumfundisha mambo ya msingi lakini hakupata hata mmoja.
Akiwa hajakatishwa tamaa, Halima aliamua mwenyewe kuangalia mitandao tofauti ili aweze kujifunza zaidi.
"Nilipitia mchakato mrefu wa kujifunza hadi kuwa mzuri zaidi," anaimbia TRT Afrika.
Halima akawa msanii kamili, mwishoni mwa 2017, akiwa na miaka 21 tu.
Halima anasifu sifa yake ya asili ya umakini kwa undani na kupenda usahihi na usawa. Anasema hii inamweka katika nafasi nzuri hata wakati mambo yanapokuwa magumu.
Urembo wa Kiafrika
Halima alifikiria jinsi bora ya kupenyeza vipengele vya kiafrika katika kazi yake.
"Niliamua kuinogesha na ladha ya kiafrika , kwa kutumia ruwaza na maumbo yenye kuwakilisha kisasa kutoka bara la Afrika. Ubinifu hauna kikomo," anasema.
Michoro yake huangazia kila kitu kuanzia misikiti hadi majengo ya rais wa Nigeria.
Michakato ya kutafakari
Kwa hivyo, mchakato wa kisanii unaoingia kwenye miundo ya Mandala ya Halima ni mgumu kiasi gani? "Kuimarika kwa mbinu hii ya sanaa kunahitaji usahihi, uthabiti, na subira. Pia unahitaji zana maalumu ya zana za Dotilism," anaeleza.
Hatua ya kwanza ya Halima kwa miradi ya mural ni kutembelea tovuti kukagua, kupima, na kuchora ramani ikiwa ni pamoja na kubainisha ubao wa rangi unaofaa.
Katika siku ya kawaida ya kazi, Halima hufika kwenye yake na kuhakikisha kila kitu kipo sawa.
Kisha, timu yake hutengeneza mpango wa michoro ikilenga kukamilisha mlingano wa wa kila kipengele cha Mandala au Tezhip.
Hufanya kazi akiwa ameketi au amesimama kwenye ngazi, kulingana na mahitaji.
"Zaidi ya motisha, sanaa ya vidoti ni mradi unaotumia wakati ambao unahitaji uvumilivu mkubwa, nidhamu, umakini, shauku kubwa na utulivu," anasema.
Ndani ya Abuja na majimbo mengi ya Nigeria, michoro ya Halima ya Tezhip na kazi za sanaa za mandala zimebadilisha nafasi za umma na za kibinafsi, hata kama zinachochea mazungumzo na hisia za utangamano na uzuri.