Uhusiano wa Afrika na mamluki wa Magharibi au makampuni binafsi ya kijeshi na usalama (PMSCs) lilianza wakati wa misafara ya biashara dhidi ya watumwa na uvamizi wa kijeshi wa enzi za ukoloni.
Kwa namna fulani, motisha za makampuni ya kijeshi ya kisasa, yanayoendeshwa na kampuni yanaakisi mienendo ya makampuni ya kikoloni ya kibinafsi yaliyotolewa katika bara na Magharibi.
Mwaka 2002, Kamati Teule ya Bunge la Uingereza Linaloshughulikia Mambo ya Nje ilitoa Waraka wa Kijani kuhusu kudhibiti makampuni ya kijeshi ya kibinafsi. Waraka hio lilikiri kwamba mamluki wa Magharibi barani Afrika hawakuwa na manufaa yoyote kwa bara hilo.
Ikinukuu vitendo vya mamluki maarufu kama vile Mwaireland Mad Mike Hoare, Mfaransa Bob Denard, na Mbelgiji Jean Schramme barani Afrika katika miaka ya 1960 na1970, waraka hio iliitaja jaribio la nchi za Magharibi "kushikilia udhibiti wa eneo lenye utajiri wa madini" kama vile "wakoloni wakijaribu kuchukua madaraka".
Mfumo usiokuwa wazi
Katika mfumo wa kisasa wa usalama wa kimataifa, Makampuni Binafsi ya Ulinzi yaliyosajiliwa kisheria "kutoa mafunzo ya usalama, ushauri na kijeshi kwa vikosi vya kijeshi na polisi wa serikali halali".
Aidha wanafanya kazi katika mfumo usioeleweka, wafanyikazi wao wakati mwingine huitwa askari huru au mamluki, kwani mara nyingi huvuka mipaka ili kujihusisha na mapigano ya kijeshi na shughuli zisizo halali au zisizo za haki za kisiasa, kiuchumi, au kifedha katika nchi ambayo wametumwa.
Miaka ya 1960 na 1970, enzi iliyofahamika kama "enzi ya dhahabu" ya wapiganaji mamluki barani Afrika, ikithibitishwa na ufafanuzi wa vigezo sita vya mamluki katika Kifungu cha 47 cha itifaki za ziada za 1977 za Mikataba ya Geneva.
Katika makala iliyochapishwa Julai 2023 katika jarida la The Standard - "How London became home to some of the world's largest private security firms" - Sophie Wilkinson anataja Aegis ya Uingereza na G4S kati ya makampuni ya ulinzi matano bora ulimwenguni.
Aegis pia inatajwa kuwa "kampuni ya kibinafsi ya pili kubwa duaniani iliyoajiri idadi kubwa baada ya Walmart, yenye uwepo katika nchi 125". Mapato ya pamoja ya kampuni hizi yana kufikia tarajiwa kufika pauni bilioni 231 za Uingerea (dola bilioni 297 za Marekani) mnamo 2026.
Kundi la Ulaya
Kampuni zingine za ulinzi za Uingereza barani Afrika ni pamoja na Aegis na G4S. Hivi majuzi, Kundi la Wagner la Urusi limejitokeza kwa wingi katika maeneo yenye mizozo ya Afrika.
Miongoni mwa makampuni makubwa ya kijeshi ya Ufaransa, Agemira inajishighulisha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Corpguard nchini Ivory Coast. Secopex imetumwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Somalia, na Libya, ambapo mwanzilishi wake, Pierre Marziali, aliuawa wakati wa mapinduzi ya 2011.
Kwa mkataba wa kuingiza pesa nchini DRC, Agemira inawaleta washauri wa kijeshi wa Kiromania na Serbia. "Kundi hilo linachukia kuitwa 'mamluki', likisisitiza kuwa wao ni wakufunzi wa kijeshi," mwandishi wa habari wa Kongo Jaffar Sabity anaiambia TRT Afrika.
Sabity anaamini kwamba Kongo na Agemira wanahofia vikwazo vya Umoja wa Mataifa, vilivyosasishwa Februari mwaka huu kuwalenga "viongozi wa kisiasa na kijeshi wa makundi ya kigeni yenye silaha yanayofanya kazi nchini DRC."
Pia anataja kwamba wachambuzi wengi wa ndani wanaamini kwamba Agemira inashiriki kikamilifu katika kupambana na waasi wa Kongo kama vile M23. "Si ajabu wana bendera ya DRC kwenye sare zao," anaeleza.
Mwanzo wa kutiliwa shaka
Mwanzo wa ubeberu wa Magharibi, mashirika mengi ya kibinafsi ya kikoloni yalisaidia kunyakua ardhi za Kiafrika kwa waajiri wao.
Baada ya vita vya Dunia vya Pili vya kuondoa ukoloni barani Afrika, jeshi la kibinafsi na makampuni ya usalama yalichochea mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi na kuwakandamiza wapigania uhuru kutoka Zambia hadi Burkina Faso.
Jaribio la mapinduzi ya mwaka 2004 nchini Equatorial Guinea, likiongozwa na wapiganaji mamluki waliofadhiliwa na mfanyabiashara Sir Mark Thatcher, mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher, liliashiria awamu mpya ya kampuni za kijeshi za Magharibi kushikilia kwa nguvu nchi za Afrika zenye rasilimali nyingi.
Hivi sasa, makampuni za ukoloni mamboleo wa Magharibi zinashutumiwa kushirikiana na makampuni makubwa yenye maslahi ya kigeni ili kuiba rasilimali za Kiafrika, kuendesha shughuli za silaha, na kuwafunza waasi kuzua migogoro na machafuko ambayo yanadhoofisha uhuru wa mataifa.
"Makampuni ya kijeshi ya kibinafsi yana hatari nyingi - ni ukoloni lakini kwa sura nyingine," mwanasheria wa Nigeria Idris Bawa, ambaye anafanya kazi kama mshauri wa kujenga amani, anaiambia TRT Afrika.
"Wanatuletea matatizo na kisha wanatushauri kuajiri mamluki ili kusaidia kutatua suala walilotutengenezea."
Bawa anapaswa kujua, kwa kuwa alikuwa sehemu ya programu ya mafunzo iliyoundwa na kampuni ya ushauri ya kijeshi ya Uingereza BMATT kwa vikosi vya kijeshi vya Nigeria.
"Zaidi ya dhahiri, kuna zaidi ya kile kinacholeta wakufunzi wa kijeshi wa kigeni barani Afrika," anaelezea.
Urithi wa wapiganaji mamluki
Hivi majuzi, serikali za Kiafrika zilizo katika mazingira magumu zilizopigwa marufuku ya silaha za Magharibi na vikwazo vya kifedha zimealika Makampuni ya Ulinzi kutoka mataifa mengine yenye nguvu ya kimataifa kama vile Urusi, China, na Uturuki kuwasaidia na dharura za usalama.
Historia yoyote ya shughuli za Makambuni ya Ulinzi barani Afrika lazima ianze na mamluki wa kifalme wa Uropa - Waingereza, Wafaransa, Wajerumani, Wareno, na kadhalika - pamoja na kampuni zilizokodishwa za kikoloni.
Kupitia utawala wa nguvu na shughuli za kidanganyifu wakishirikiana na machifu wa asili wa Kiafrika, makampuni ya mamluki ya kikoloni yalianza unyonyaji, unyakuzi, na ugawaji wa ardhi za Kiafrika kwa kutumia hoja ya kukabiliana na biashara ya watumwa, na baadaye kwa unyonyaji wa rasilimali za Kiafrika na shughuli za kimishonari.
Zimbabwe na Zambia ni mifano miwili ya nchi za Kiafrika ambazo zilifufuka tena baada ya kuatihiriwa na makampuni ya mamluki ya Uingereza, yaliyopewa jukumu la kukamata, kusimamia, na kudai makoloni ya ng'ambo barani Afrika kwa niaba ya mfalme la Uingereza.
Nchi hizo mbili za kusini mwa Afrika ziliwahi kuitwa The Rhodesias, jina ambalo kwa ujasiri lilikuwa na alama mahususi ya Cecil Rhodes, mamluki maarufu wa kifalme wa Uingereza na mkombozi wa kusini mwa Afrika.
Kufuatia unyakuaji wa Rhodes mwaka wa 1889 kupata ruhusa ya Kifalme iliyompa mamlaka ya kunyonya utajiri wa madini wa Zambesia iliyokufa, alianzisha Kampuni ya Uingereza ya Afrika Kusini, hivyo akaweka misingi ya jimbo jipya la kifalme ambalo baadaye lingeitwa jina lake.
Haya yaliandikwa katika kitabu cha 'Stephen Alexander Massie The Imperialism of Cecil John Rhodes', ambacho kinasimulia historia ya kuyataja maeneo yanayozunguka Mto Zambezi kama "Rhodesia Kaskazini" na "Rhodesia ya Kusini". Hatimaye walipata uhuru - Zambia mwaka 1964 na Zimbabwe mwaka 1980.
Katika kitabu chake, The Trial of Cecil John Rhodes, mwandishi wa riwaya wa Nigeria Adekeye Adebajo anaandika, "Ilisemwa mara nyingi wakati wa enzi ya kifalme kwamba biashara ilifuata bendera. Rhodes, kwa kweli, aligeuza hili, na serikali ya Uingereza ikifuata uongozi wake na kutoa mikopo, msaada wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi kwa mamluki wake na wafanyabiashara."
Mnamo 1898, utawala wa kifalme wa Uingereza uliidhinisha rasmi uvamizi na jina la Rhodesia, ambayo walowezi walikuwa wameikubali kwa njia isiyo rasmi tangu 1890.
Shujaa mwenye sifa mbaya
Licha ya kupewa kwake daraja ya juu hadi kuwa ushujaa, kiambishi awali "mamluki" hakiwezi kutenganishwa na mkoloni wa pili maarufu wa Uingereza barani Afrika, Baron Frederick Lugard. Mwanajeshi huyo wa zamani na mamluki asiye na haya aliwahi kuwa msimamizi wa kikoloni katika kanda mbalimbali za Afrika Mashariki na Magharibi.
Baada ya kuhudumu katika 'British India', Kapteni Lugard aliongoza msafara wa wanajeshi binafsi na wafanyabiashara waliotumwa Afrika. Hatimaye alijihusisha na nchi kadhaa, kutoka Sudan hadi Nigeria na Tanzania hadi Malawi.
Katika tasnifu yake iliyonukuliwa sana kuhusu kuzingatiwa upya kwa maadili ya sera za kikoloni za Uingereza katika Afrika mashariki, mwanahistoria wa Norway Jonas Fossli Gjersø anaandika kuhusu jinsi Lugard alivyohusika katika kutumia makampuni ya mfalme yaliyoendeshwa na mishale ya mamluki kama zana za ukoloni.
Mfano mmojawapo ni mkataba uliotiwa saini na Kampuni ya Lugard ya Imperial British East Africa mnamo Desemba 1890 na Kabaka (Mfalme) Mwanga II wa Buganda, ambao uliweka ufalme chini ya ulinzi wa kampuni hiyo.
Kuanzia 1894 na kuendelea, Lugard alihusika na makampuni mengine ya kikoloni ya Uingereza, kama vile Kampuni ya Royal Niger katika Nigeria, Kampuni ya British West Charterland Botswana, na African Lakes Corporation Malawi na Msumbiji.
Kuzaliwa upya baada ya Vita Vya Dunia Vya Pili
Nakala ya Wilkinson inaelezea jinsi "vita vidogo katika mataifa maskini vilisababishwa na kuongezeka kwa kampuni za kijeshi za kibinafsi za Uingereza" katika miaka ya 1960 na 1970.
Majeshi ya mamluki na washirika wa chini kwa chini kwa nguvu za kikoloni walikuwa wahusika wakubwa katika "kukandamiza uasi na kuchochea machafuko".
Kulingana na ripoti ya Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza, mwisho wa Vita Baridi ulileta ziada ya wanajeshi wa zamani walioajiriwa na makampuni kama Sandline na Executive Outcomes, ambao walipigana na waasi nchini Sierra Leone na Angola.
Kama Sabity anavyotaja, wanajeshi wa kigeni kwa muda mrefu wameingilia masuala ya mataifa ya Afrika ya Kati - katika kesi ya DRC, tangu kuwepo kwa mamluki wa Ubelgiji Schramme katika Zaire ya zamani ya Mobutu Sese Seko.
Mwandishi huyo wa habari pia anataja madai ya mamluki wa Kiingereza, Australia, na Israeli ambao bado wanafanya kazi katika eneo la waasi la M23.
Wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Nigeria vya miaka ya 1960, mamluki wa Ufaransa na Israeli walilaumiwa kwa kuchangia kurefusha vita hivyo, vilivyodumu kwa miezi 30.
Mzunguko wa ukoloni mamboleo
Mwisho wa Vita Baridi, mwanzoni mwa miaka ya 1990 ulileta sura mpya kwa makampuni binafsi ya ulinzi, kwani mamilioni ya askari waliofukuzwa walitafuta kazi za kibinafsi, wakati Afrika ilikuwa imekumbwa na migogoro ya muda mrefu ya kikanda.
Migogoro ya Afrika kuanzia miaka ya 1990 hadi 2020 ilijumuisha ile ya Sudan, Libya, Mali, Chad, Burundi, Sierra Leone, Nigeria, Eritrea, Uganda, Rwanda, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kongo DR, Angola, Somalia, Algeria, Ivory Coast, Liberia na kadhalika.
Mnamo 1989, Eeben Barlow, kanali mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini la enzi ya ubaguzi wa rangi, alianzisha Executive Outcomes, ambayo ilipigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sierra Leone.
Kampinu ya Dyck Advisory Group, iloanzishwa mwaka wa 2012 na mwanajeshi mzungu wa Zimbabwe Kanali Lionel Dyck, ilipigana dhidi ya Al-Shabaab nchini Msumbiji mwaka wa 2020.
Makampuni binafsi nyingi za kisasa zinazofanya kazi - ikiwa ni pamoja na Osprey, Blackhawk, MPRI, CACI International, DynCorp, Triple Canopy, AdvanFort, Xeless, na Asgaard - hufanya kazi kivyake katika maeneo yote ya Afrika, kutoka Misri hadi Mauritania.
Bawa kwa kiasi fulani analaumu mataifa ya Afrika kwa kutia saini mikataba ya kijeshi ambayo inawapa watendaji binafsi wa kijeshi wa Magharibi fursa ya moja kwa moja kutembelea na kukagua vituo vya kijeshi vya serikali, kufichua siri za serikali na kuwezesha kuenea kwa makampuni binfafsi ya ulinzi katika bara hilo.
Uchumi unaostawi wa migogoro upo katika maeneo yenye matatizo ya Afrika na unahusishwa kwa karibu na uchumi mpana wa kisiasa wa kimataifa. Maslahi na ajenda za ukoloni mamboleo wa Magharibi zimejikita kwa kina katika migogoro hii.
Sio tena suala la wafanyabiashara wa silaha wa Magharibi kutafuta uuzaji wa silaha na kandarasi za kijeshi kutoka kwa serikali za Kiafrika. Miguu ya ukoloni mamboleo yatasalia ardhini mradi mataifa dhaifu yatasalia kutokuwa na usalama, kutokuwa na utulivu na tayari kuachilia mamlaka ya nchi yao.