Mahakama ya kijeshi ya Niger ilimruhusu Mohamed Bazoum Salem, mtoto wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum, kuachiliwa kwa muda kutoka katika kifungo cha nyumbani katika mji mkuu wa Niamey siku ya Jumatatu, ilisema katika taarifa yake.
Salem, 23, amekuwa kizuizini katika makao ya rais na wazazi wake tangu baba yake alipopinduliwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi mwezi Julai.
Mapinduzi hayo, ambayo ni moja kati ya nane za Afrika Magharibi na Kati tangu mwaka 2020, yalilaaniwa na watu wengi, na kusababisha vikwazo kutoka kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), na kusababisha wito mkubwa wa kuachiliwa kwa Bazoum na kurejea katika utawala wa kidemokrasia.
Jeshi hlikutoa maelezo kuhusu hatima ya wazazi wa Salem.
Uamuzi wa mahakama ya ECOWAS
Mwezi uliopita, Mahakama ya Haki ya ECOWAS iliamua kwamba kuwekwa kizuizini kwa familia hiyo ni kinyume cha sheria na kuamuru kurejeshwa kwa Bazoum. Mahakama, ambayo maamuzi yake hayawezi kukata rufaa, imewapa utawala wa kijeshi wa Niger mwezi mmoja kusema jinsi itakavyotekeleza agizo hilo, mawakili hao walisema.
Bazoum na mwanawe walishtakiwa baada ya mapinduzi ya Julai 26. Salem alishtakiwa kwa kula njama kwa lengo la kudhoofisha mamlaka au usalama wa serikali.
Familia hiyo haijapata maji wala umeme, kulingana na chama cha Bazoum na jamaa zao. Mawakili wa familia hiyo hapo awali walisema hawajaruhusiwa kukutana na hakimu au kufahamishwa kuhusu taratibu zozote za kisheria dhidi yao.