Judith Suminwa pia alikumbusha changamoto ambazo wanawake wa Kikongo na wa Afrika

Na Kudra Maliro

TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa ameorodheshwa kama mwanamke wa 77 mwenye kuvutia zaidi duniani katika orodha maarufu ya Jarida la Forbes.

Tangazo hilo lilitolewa kupitia akaunti yake rasmi ya X Jumatatu. Kutambuliwa kwa Suminwa na Forbes ni sehemu ya harakati za kimataifa za kusherehekea na kuhamasisha wanawake viongozi katika maeneo mbalimbali. Uteuzi wa Suminwa pia ni ishara muhimu kwa vizazi vijavyo, kwani unaonyesha kuwa uongozi wa kike sio tu unawezekana, bali pia unaweza kutambuliwa na kusherehekewa duniani kote.

“Kuteuliwa kuwa mwanamke wa 77 mwenye nguvu zaidi duniani na Forbes ni zaidi ya utambuzi binafsi: ni ishara ya matumaini kwa kila msichana na mwanamke wa Kikongo,” aliandika Waziri Mkuu kwenye X.

Judith Suminwa pia alikumbusha changamoto ambazo wanawake wa Kikongo na wa Afrika wanakutana nazo katika juhudi zao za uongozi ubora.

Licha ya vikwazo vingi, uteuzi huu, anasema, unaonyesha kuwa uongozi wa kike ni hali halisi inayowezekana na inahitajika katika maeneo yote.

Aliongeza kwamba uteuzi huu unaonyesha kuwa wanawake wana uwezo wa ubora na uongozi. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliorozeshwa nafasi ya 91 na jarida hilo.

Jarida la Forbes linajulikana kwa orodha zake mbalimbali zinazochapishwa kila mwaka.

TRT Afrika