Jamii ya Faru weupe iko hatarini kutoweka. / Picha: Getty Images  

Na Charles Mgbolu

Afrika Kusini imelenga kuwarejesha Faru weupe 2000 ndani ya miaka 10 ijayo. Zoezi hilo litaratibiwa na shirika la uhifadhi la African Parks likishirikiana na Serikali ya Afrika Kusini.

Kulingana na shirika hilo, zoezi la ufugaji wa wanyama hao litasitishwa pindi Faru hao wakirejeshwa.

Zoezi hilo, linatajwa kuwa la hatari, huku wahifadhi wakiwa wamejipanga kuhakikisha hakuna kasoro yoyote itakayojitokeza wakati wa utekelezaji wake.

Jamii ya Faru weupe wanaopatikana Afrika Kusini wako hatarini kutoweka kutokana na ujangili.

Wahifadhi wako makini kuhakikisha kuwa hakuna kasoro itakayojitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo. Picha:  Getty Images

“Shirika la African Parks halina nia ya kuhodhi mradi ya kuzalisha Faru 2,000. ''Hata hivyo, tunatambua umuhimu wa kutafuta suluhisho kwa wanyama hawa wanaporudi kwenye ikolojia zao,” anasema Peter Fearnhead, Afisa Mtendaji Mkuu wa African Parks.

“The scale of this undertaking is simply enormous, and therefore daunting. However, it is equally one of the most exciting and globally strategic conservation opportunities,” Fearnhead added.

“Ukubwa wa zoezi hili una changamoto yake. Hata hivyo ni kati ya vitu muhumi sana katika fursa za kiuhifadhi,” Fearnhead anaongeza.

Zoezi hili linaweza kuwa la kuvutia sana.

Taasisi ya Your Perfect Africa ya Afrika Kusini, anatoa picha ya zoezi hili.

Baada ya muhtasari wa mambo ya kufanya na kutofanya, kikosi kazi kinachohusisha wahifadhi na madaktari wa wanyama, hupelekwa kwenye eneo la faru wengi waliogundulika toka angani.

Kwa msaada wa helikopta yenye rubani mzoefu, Faru hao hutenganishwa katika makundi na kudungwa sindano za usingizi.

Baada ya sindano hiyo, Faru hukimbia kwa dakika 6 hadi 8 kabla ya kudondoka na kupoteza fahamu na kikosi kazi hicho huanza kazi yake.

Faru hao hutenganishwa kutoka angani./Picha: Getty Images

Kila mtu, lazima afanye kazi kwa hara sana kwa wakati huu.

Kisha, kitambaa hufungwa machoni mwa faru na soksi kwenye masikio ili kuzuia usumbufu wa aina yoyote wakati wa ukusanyaji wa taarifa kutoka kwa viumbe hao na kuanza kuwafuatilia.

Baada ya hapo, wanyama hao hufungwa visukuma mawimbi na kupelekwa sehemu ya kutokea.

Faru weupe wa Afrika Kusini ni kati ya jamii ndogo iliyosalia duniani, ambao wako hatarini kutoweka, linasema shirika la Africa Parks.

Shirika hilo linasema kuwa kila Faru atakayerudishwa kwenye maeneo yaliyohifadhiwa barani Afrika, watachangia kwenye uendelevu wa ikolojia kama vile mzunguko wa lishe, kukuza utalii na mapato kwa wananchi.

TRT Afrika