Jumapili, Mach 31, 2024
2200 GMT — Rais wa Türkiye Recep Tayyip Erdogan amesema matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa yaliashiria "mabadiliko" kwa Chama chake cha Justice and Development (AK Party).
Licha ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Erdogan aliahidi "kuheshimu uamuzi wa taifa."
Akihutubia umati wa watu kutoka makao makuu ya chama katika mji mkuu Ankara, Erdogan alisema chama chake hakingeweza kufikia matokeo yaliyotarajiwa kutoka uchaguzi wa mitaa wa Jumapili. .
"Tutatathmini matokeo ya uchaguzi wa ndani kwa moyo wa wazi katika chama chetu na tutajihusisha na kujikosoa," Erdogan alisema
2040 GMT - Imamoglu wa Upinzani atangaza ushindi huko Istanbul
Meya wa sasa wa Istanbul na mgombea wa chama cha upinzani CHP Ekrem Imamoglu ametangaza ushindi katika mji mkubwa wa Uturuki wa Istanbul.
1620 GMT ( Saa moja na dakika ishirini jioni) — marufuku ya uchapishaji uchaguzi imeondolewa.
Mwenyekiti wa Baraza la Juu la Uchaguzi (YSK), Ahmet Yener, alitangaza kwamba marufuku ya uchapishaji kuhusu uchaguzi imeondolewa.
1430 GMT ( Saa kumi na moja unusu za jioni)
Rais wa Baraza Kuu la Uchaguzi la Uturki (YSK), Ahmet Yener, alisema, "Mchakato wa upigaji kura, ambapo wapiga kura milioni 61 441 elfu 882 wamepiga kura zao katika masanduku ya kura 207 elfu 848, na vyama 34 vya kisiasa vikishindana, umekamilika bila shida isipokuwa kwa matukio machache kadhaa," rais wa Baraza Kuu la Uchaguzi la Türkiye (YSK) alisema.
"Taratibu za kuhesabu kura na uwekaji nyaraka zimeanza, na taarifa za matokeo ya kisanduku zimeanza kuingizwa kwenye mfumo, huku mtiririko wa data ukiendelea," Ahmet Yener alisema.
"Bodi itakutana hivi karibuni kutathmini suala hilo na kuamua juu ya marufuku ya uchapishaji."
1400 GMT( Saa kumi na moja jioni)— Upigaji kura umekamilika kote nchini Uturuki katika uchaguzi wa serikali za mitaa
Upigaji kura ulianza saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na moja jioni katika sehemu kubwa ya nchi.
Kwa sababu ya hali ya msimu na nyakati za machweo mwezi Machi, YSK imesogeza saa za kupiga kura saa moja mbele katika mikoa 32 ya mashariki.
Katika majimbo hayo ya mashariki, saa za kupiga kura zilikuwa kutoka saa moja asubuhi hadi saa kumi jioni.
1234 GMT ( Saa tisa na dakika 34 mchana)
Mgombea wa umeya wa chama tawala cha AK mjini Istanbul, Murat Kurum, ametoa wito kwa wananchi wote kupiga kura na kulinda masanduku ya kura.
"Ninawaita wananchi wote kupiga kura na kulinda masanduku ya kura. Waache waende wapige kura zao na walinde masanduku ya kura," Kurum alisema, baada ya kupiga kura yake na familia yake.
Kurum alitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kuondoka.
Alitoa shukrani kwa wananchi kwa kumpokea kama kaka na mtoto wao huku akishiriki miradi na ndoto zake na wananchi wa Istanbul katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
"Natamani kura yetu italeta wema kwa Istanbul, nchi yetu na taifa letu," alisema.
1144 GMT ( saa nane na dakika 44 mchana) — Meya wa Istanbul Imamoglu amepiga kura
Meya wa Manispaa ya Metropolitan (IBB) Ekrem Imamoglu alipiga kura yake mjini Beylikduzu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa unaofanyika Machi 31.
“Natumai tutaafikiana na matokeo ya sanduku la kura yatakayoibuka kwenye uchaguzi na watu wetu milioni 16. Bila shaka tukiwa na mamlaka tunatumai tutaendelea kulitumikia jiji letu kwa njia bora zaidi kwa miaka 5 ijayo, " alisema.
Alieleza kuwa atafuatilia matukio yanayohusiana na uchaguzi katika makao makuu ya mkoa wa chama chake, alieleza nia yake ya mchakato huo kumalizika kwa utulivu.
1030 GMT ( saa saba unusu mchana)
Uchaguzi wa serikali za mitaa "utaashiria mwanzo wa enzi mpya katika nchi yetu," Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema baada ya kupiga kura yake mjini Istanbul pamoja na mke wake Emine Erdogan.
Erdogan ambaye taaluma yake ya kisiasa ilianza kama meya wa Istanbul mwaka 1994, pia alitaja uchaguzi wa mwaka jana wa bunge na urais ambao ulipigwa vita vikali na anatumai kuwa "hizi zitakuwa muhimu katika mwanzo wa enzi mpya, karne mpya katika nchi yetu."
Baada ya kupiga kura katika wilaya ya Uskudar ya jiji hilo, Erdogan alisisitiza umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi huo, akiwataka raia wote wanaostahili "kujitokeza na kufanya chaguo lao."
0500 GMT ( Saa mbili za asubuhi) — uchaguzi wa serikali za mitaa waanza Uturuki
Upigaji kura ulianza kote Uturuki siku ya Jumapili ili kuwachagua mameya wa jiji, mameya wa wilaya, na maafisa wengine wa eneo hilo ambao watahudumu kwa miaka mitano ijayo, ikiwa ni pamoja na katika miji yenye ushindani mkali ya Istanbul, Ankara, na Izmir.
Upigaji kura ulianza saa 7 asubuhi kwa saa za hapa nchini na utaendelea hadi saa kumi jioni katika majimbo 32 ya mashariki, na katika majimbo yaliyosalia, vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 8 asubuhi na kufungwa saa 5 jioni.
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Machi 31, zaidi ya wapiga kura milioni 61 kote nchini wanastahili kupiga kura katika vituo zaidi ya 200,000 huku wagombea kutoka vyama 34 vya siasa wakishindana.
Vyama vikuu vinavyoshindana ni chama tawala cha Justice and Development (AK) Party, chama kikuu cha upinzani cha Republican People's Party (CHP), Nationalist Movement Party (MHP), Good (IYI) Party, na Peoples' Democratic Party (DEM Party) .
Wapiga kura wanaweza tu kuwapigia kura wagombeaji wa ofisi katika wilaya zao. Baadhi ya vijana milioni 1.32 watapiga kura kwa mara ya kwanza.
Karatasi ya kura ya Istanbul ina wagombea 49.
Zaidi ya masanduku 1,000 ya kupigia kura yanayohamishika yataundwa kwa ajili ya wapiga kura ambao hawawezi kwenda kwenye uchaguzi kwa sababu ya ugonjwa au ulemavu.
Siku ya uchaguzi, uuzaji na unywaji wa aina zote za vileo vitapigwa marufuku kabisa katika maeneo yote yanayotoa pombe na kumbi za umma kuanzia saa 6 asubuhi hadi saa sita usiku wa manane.
Vituo vya redio na utangazaji haviruhusiwi kutoa habari, ubashiri au maoni kuhusu matokeo ya uchaguzi au uchaguzi hadi saa 12 jioni (1500 GMT).
Kuanzia saa 12 hadi saa 3 jioni (1500-1800 GMT), matangazo yanayohusiana na uchaguzi yanaweza tu kutumia habari na matangazo kutoka kwa Baraza Kuu la Uchaguzi (YSK).