Wanajeshi wa ulinzi wa rais wamemuondoa madarakani kiongozi wa Niger Mohamed Bazoum, kutokana na hali ngumu ya kiuchumi na ukosefu wa usalama. Picha: Reuters

Viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger wamesema kuwa chombo cha kikanda cha ECOWAS kinaweza kuanzisha uingiliaji kati wa kijeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Sahel.

Akizungumza kabla ya mkutano wa ECOWAS kuhusu Niger siku ya Jumapili, mamlaka ya kijeshi ilisema: "Lengo la mkutano huu ni kuidhinisha mpango wa uchokozi dhidi ya Niger, kwa njia ya uingiliaji wa kijeshi unaokaribia huko Niamey, kwa ushirikiano na nchi za Kiafrika ambazo sio wanachama wa baraza la kikanda na mataifa fulani ya Magharibi."

Awali jeshi viongozi hao wa kijeshi walikuwa wametahadharisha dhidi ya hatua yoyote ya kijeshi kutoka kanda hilo.

Mkutano wa kikanda wa ECOWAS unaendelea mjini Abuja Nigeria kwa mualiko wa rais Tinubu, ambapo ajenda kuu ni kuangazia tatizo la Niger na kutafutia suluhu.

TRT Afrika