MONUSCO, umekabiliwa na maandamano tangu mwaka jana yaliyochochewa na malalamiko kwamba umeshindwa kuwalinda raia. / Picha : AFP

Wanajeshi sita walishtakiwa Jumanne kwa kuhusika kwao katika mauaji ya watu 56 wakati wa msako wa jeshi dhidi ya waandamanaji waliopinga uwepo wa UN, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki iliyopita.

Kundi hilo, ambalo linajumuisha kanali na luteni kanali kutoka kwa walinzi wa Jamhuri, wanashitakiwa kwa "uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kufanya mauaji, uharibifu wa nia mbaya na kuchochea askari kufanya vitendo kinyume na wajibu au nidhamu", kulingana na taarifa ya jeshi mahakamani mjini Goma.

Maafisa hao wawili walikuwa wakuu wa wanajeshi waliowapiga risasi waandamanaji, kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na ofisi ya rais ambacho kiliomba kutotajwa jina.

"Hii haikuwa hatua ya serikali, walijitenga tena haiko katika mfumo wa misheni zao huru," mwendesha mashtaka wa kijeshi Michel Kashil aliiambia mahakama.

"Tutadhihirisha kwamba hili ni shambulio la kimfumo dhidi ya watu waliolengwa vyema, washiriki wa kanisa fulani," alisema.

Awali serikali ya Congo ilikuwa imesema watu 43 waliuawa katika machafuko ya Goma Jumatano iliyopita. Katika kesi hiyo, mwendesha mashtaka Kashil alisema idadi ya waliofariki ilifikia 56, huku watu wengine 75 wakijeruhiwa.

Chuki dhidi ya MONUSCO

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Kongo, unaojulikana kama MONUSCO, umekabiliwa na maandamano tangu mwaka jana yaliyochochewa na malalamiko kwamba umeshindwa kuwalinda raia dhidi ya miongo kadhaa ya ghasia za wanamgambo.

Maandamano ya kupinga MONUSCO mnamo Julai 2022 yalisababisha vifo vya zaidi ya 15, wakiwemo wanajeshi watatu wa kulinda amani huko Goma na mji wa Butembo.

Reuters
TRT Afrika