Chuo kikuu chenye kuelea baharini kimewasili mjini Mombasa, Kenya.
Meli hiyo ya kitalii imewasili katika pwani ya Mombasa, Mamlaka ya Bandari ya Kenya imesema.
Chuo kikuu hicho chenye kuelea majini kiliwasili mjini Mombasa, Februari 9, na kitatia nanga kwenye mji huo kwa siku sita.
Meli hiyo, MV World Odyssey, maarufu kwa jina la "Semester at Sea" inachukua wanafunzi wa shahada ya kwanza, na wa hivi karibuni kusomea baharini, elimu ambayo pia inahusisha kusafiri kwenda nchi tofauti kujifunza historia na tamaduni zao.
"Ndani ya meli hiyo kuna abiria 763, kati yao 585 ni wanafunzi ambao watatembelea vyuo vya elimu ya juu kwa ziara za kielimu, kufanya matembezi kuzunguka majiji, na kutembelea mbuga mbalimbali za wanyama wakati wa ziara yao," Mamlaka ya Bandari ya Kenya ilisema kupitia ukurasa wake wa X.
Ijulikanayo kama kampasi kubwa zaidi ieleayo majini, meli hiyo imekuwa ikitembelea Kenya kuanzia mwaka 2022.
Bandari ya Mombasa imerekodi ongezeko la za kitalii, huku bandari hiyo ikipokea abiria 2500 ndani ya MSC Poesia, Februari 3, moja ya meli kubwa kuwahi kutia nanga bandarini hapo.