Kikundi cha wanajeshi nchini Niger kimetangaza wao ndio viongozi wa serikali,
Rais Bazoum hajaonekana tangu 26 Julai wakati wanajeshi walimteka ndani ya kasri lake jijini Niamey.
Umoja wa Afrika imetoa amri kwa wanajeshi kurudisha uongozi kwa raia. Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limefanya mkutano Ijumaa kujadili mapinduzi ya serikali nchini humo.
Umoja wa Afrika inapinga mageuzi ya serikali ambayo hayafanyiki kupitia uchaguzi.
Je, Umoja wa Afrika umefanya maamuzi gani?
Inawataka wanajeshi kurudi mara moja na bila masharti katika kambi zao na kurejesha mamlaka kwa rais aliyeteuliwa kikatiba ndani ya muda usiozidi siku kumi na tano (15) kuanzia tarehe 28 Julai.
Pia imeamuru kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa rais Mohamed Bazoum na wafungwa wengine wote.
Umoja wa Afrika umetaka wanajeshi nchini Niger wadumishe heshima ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa afya za rais na familia yake.
Baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika, limeonya kwamba litachukua hatua zinazohitajika, pamoja na hatua za adhabu dhidi ya wahusika wa mapinduzi ya serikali iwapo haki za wafungwa wa kisiasa hazitaheshimiwa.
Jumuia ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, chini ya uenyekiti wa rais wa Nigeria Bola Tinubu imefuatilia kwa makini mapinduzi ya serikali nchini Niger,
Imemtuma rais Patrice Talon, wa Jamhuri ya Benin kama Mjumbe maalum nchini Niger.
Maraia wa nchi wanachama wa ECOWAS wamepanga kufanya mkutnao kujadili hali ya Niger tarehe 30 Julai 2023 mjini Abuja, Nigeria