Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune akihutubia taifa katika sherehe ya uapisho iliyofanyika ikulu Algiers, Algeria, Disemba, 19, 2019. / Picha: AP

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ameilaumu vikali Ufaransa kwa athari zilizobaki za utawala wa kikoloni nchini Ufaransa.

Lawana hizo zimekuja wakati wa hotuba iliyotolewa katika mabunge mawili wakati wa kuhutubia taifa ambapo alielezea mafanikio yake katika muhula wa kwanza wa urais wake kuanzia 2019-2024 na kuainisha mpango wake kwa muhula wa pili, ambao umeanza Septemba, kwa mujibu wa mwandishi wa Anadolu.

Tebboune amesema Algeria inataka kwamba Ufaransa kukiri uhalifu uliofanya katika kipindi cha ukoloni kuanzia 1830-1962, na kusisitiza kwamba, nchi haitaki kulipwa fidia.

"Tunafuatilia heshima ya wazee wetu," amesema.

"Idadi ya raia wa Algeria waliouawa kipindi chote za miaka 132 ya ukoloni ni milioni 5.6, hakuna kiwango cha fedha kinachoweza kufidia hata kwa mtu mmoja aliyeuawa katika kipindi cha mapambano,” amesisitiza.

'Mauaji ya halaiki'

Kauli hii inakuja kukiwa na mgogoro wa kisiasa kati ya Algeria na Ufaransa ambao umesababisha kuondolewa kwa balozi wa Algeria na kuitwa kwa balozi wa Ufaransa.

Mamlaka ya Algeria imehusisha kudodora kwa uhusiano na "vitendo vya kikatili vya Ufaransa katika ardhi ya Algeria."

Tebboune also recalled the atrocities committed by the French colonial army, particularly under General Thomas Robert Bugeaud, governor-general of Algeria from 1841-1847, whom he described as "genocidal."

Amerudia msisitizo wake katika kuangalia mafaili ya Ufaransa na kusema kuwa Ufaransa unaendelea kuzuia makuvu 500 ya Waalgeria ambao walikatwa vichwa katika karne ya 19 na kupelekwa Paris.

"Tumefanikiwa kupata mkuvu 24 tu mpaka sasa," amesema.

Tebboune pia ametangaza mpango wa kuanzisha mazungumzo na vyama vya siasa mwanzoni mwa mwaka ujao "kudumisha umoja."

Amesema mazungumzo, ambayo tarehe ya kuanza haijatangazwa, yatakuwa "ya kina," yakifikia kilele cha kuanzishwa kwa sheria mpya kuhusu vyama vya siasa na asasi.

TRT World