Waandamanaji hao walikemea tamko la jenerali wa Israel anayedaiwa kuwafananisha Wapalestina na wanyama./ Picha : TRT Afrika 

Viongozi mbali mbali kutoka Kenya wameshutumu kil ewalichoita ubaguzi wa wazi unaofanywa dhidi ya Wapalestina wakati wao ndio wanaopokea 'vipigo vya dhulma' kutoka kwa Israel.

Wanasiasa pamoja na viongozi wa kidini kutoka mji wa Mombasa, Pwani ya Kenya waliongoza maandamano ya amani Jumamosi katikati mwa jiji wakipinga unyanyasaji wa Wapalestina mikononi mwa Waisraeli.

'Kwa siku kumi na tano Waisraeli wamefanya mashambulio na kuwaua wanawake na watoto wasio n ahatia katika jela kubwa zaidi ya wazi duniani,'' amesema Mohammed Ali, Mbunge wa Nyali, jijini Mombasa. 'Dunia nzima imekaa kimya na kutazama. Sio Palestine pekee, mahala popote panapotokea dhulma tunatakiwa kukemea,'' aliongeza mbunuge huyo.

'Uhuru Kwa Palestine!!! Uhuru kwa Palestine!!!'' waliimba mamia ya watu waliojitokeza katika maandamano hayo ya mchana.

Kupigania Uhuru wa Palestine

'Tumeona viongozi kutoka Marekani, akiwemo Rais wao, ameenda Tel Aviv kuwafariji Waisraeli. Tumeona viongozi wengine pia wamekimbilia Waisraeli. Hakuna hata kiongozi mmoja amefika kuangalia madhila ya Wapalestina,' ameongeza Mbunge Mohammed Ali.

Waandamanaji wameshutumu vyombo vya kimataifa kwa ubaguzi linapokuja suala la Palestine licha ya mauaj yanayofanywa dhidi yao na Waisraeli / Pich a: TRT Afrika 

Waandamanaji hao walikemea tamko la jenerali wa Israel anayedaiwa kuwafananisha Wapalestina na wanyama.

'Hata sisi tuliwahi kupigania uhuru wetu hapa Kenya, tulikuwa na Mau-mau walioongoza juhudi hizo. Wakaitwa magaidi, mpaka wakajikombo an akulikomboa taifa.' Alisema mbunge Mohammed Ali.

Miongoni mwa malalamiko kutoka kwa waliohutubia maandamano hayo ni kwa nchi za Kiislamu wamaboa walilaumiwa kwa kuona yanayoendelea huko Palestine na kutochuku ahatua zozote za maana.

TRT Afrika