Yahya Sinwar alitangazwa kama kiongozi wa Hamas kufuatia kifo cha kiongozi wa zamani, Haniyeh/ Picha: AP  

Vyombo vya haabri vya Israeli vimeripoti kuwa kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar aliuwawa huko Gaza.

Vyombo hivyo, KAN na N12 News viliwanukuu maofisa wa Israeli siku ya Alhamisi, vikisema kuwa Sinwar amekufa.

Hata hivyo, hapakuwa na uthibitisho wowote kutoka kwa Hamas.

Awali, jeshi la Israeli lilisema kuwa lilikuwa linaangalia uwezekano wa kuwa limemuua Sinwar, kufuatia tukio la uvamizi wa Gaza ambao ulilenga wapiganaji wa Kipalestina.

Sinwar alitangazwa kama kiongozi wa Hamas kufuatia kifo cha kiongozi wa zamani, Ismail Haniyeh kilichotokea Tehran, mwezi Julai.

Sinwar alikuwa anatafutwa na Israeli, huku Tel Aviv ikimtuhumu kwa kusuka mipango ya uvamizi wa mpakani wa Oktoba 7, uliosababisha mashambulizi ya mwaka mzima dhidi ya Gaza yalioua zaidi ya watu 45,000, kulingana na mamlaka za afya.

Kwa sasa, sehemu kubwa ya Gaza imegeuka kuwa magofu kufuatia mashambulizi ya Israeli, kukiwa na zuio kubwa la upatikanaji wa chakula, maji safi na madawa.

Jeshi la Israel limesema hakuna dalili zozote kwamba mateka walikuwepo katika jengo ambalo watatu hao waliuawa.

TRT Afrika