Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilimetaka kusitishwa mara moja kwa mauzo yote ya silaha kwa Israel.
Baraza hilo limeangazia onyo la "mauaji ya halaiki" katika vita Israel huko Gaza, ambavyo vimeua zaidi ya watu 33,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Azimio hilo ambalo lilipitishwa na nchi 28 kati ya 47 wanachama wa baraza hilo kwa kura ya 'Ndio', huku kupiga kura ya ndio, sita zilipinga na 13 hazikupiga kura.
Hii ni mara ya kwanza kwa chombo hicho cha Umoja wa Mataifa kuonesha msimamo kuhusu umwagaji damu unaoendelea dhidi ya watu wa Palestina.
Azimio hilo lilisisitiza "haja ya kuhakikisha uwajibikaji kwa ukiukaji wote wa sheria za kimataifa za kibinadamu na sheria za kimataifa za haki za binadamu ili kukomesha hali ya kutokujali".
Kufukuzwa kwa Israeli
Pia ilieleza "wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuibuka kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu".
Israel ilitupilia mbali azimio la Umoja wa Mataifa na kuiita kama "hoja isiyo na msingi".
Meirav Eilon Shahar, mwakilishi wa kudumu wa Israel ndani ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, alilishutumu Baraza hilo kwa "kuwatelekeza watu wa Israel kwa muda mrefu na kutetea Hamas kwa muda mrefu".
Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, ambalo hukutana mara kadhaa kwa mwaka, ndilo chombo pekee cha kiserikali kilichoundwa kulinda haki za binadamu duniani kote.
Baraza hilo lina mamlaka ya kuongeza uchunguzi wa rekodi za haki za binadamu za nchi na kuidhinisha uchunguzi.