Shambulio la anga la Israeli dhidi ya Beirut ya Lebanon / Picha: Reuters

Israeli imeanza upya shambulio la angani kwenye vitongoji vya kusini mwa Beirut katika kile ambacho jeshi la Israeli lilisema ni kulipiza kisasi kwa shambulio la kombora siku tatu zilizopita.

Kulingana na ripoti za awali kutoka kwa vyombo vya habari vya serikali ya Lebanon, mwanamke mmoja ameuawa na wengine saba wamejeruhiwa.

Mlipo mkubwa ulisikika na moshi mkubwa ulionekana ukipanda juu ya vitongoji vya kusini - ngome ya Hezbollah - mnamo saa 1640 GMT, shahidi wa Reuters alisema.

Chanzo kikuu cha usalama cha Lebanon kilisema kamanda mwandamizi wa Hezbollah alikuwa mlengwa wa shambulio la angani na hatima yake haijafahamika.

Shirika la habari la kitaifa la Lebanon linaloendeshwa na serikali lilisema shambulio la angani la Israeli lililenga eneo karibu na Baraza la Shura la Hezbollah katika kitongoji cha Haret Hreik cha mji mkuu.

Beirut imekuwa katika hali ya tahadhari kwa siku kadhaa mbele ya shambulio la Israeli lililotarajiwa kama kisasi kwa shambulio la roketi katika Milima ya Golan siku ya Jumamosi.

Hezbollah imekana kuhusiku na mashambulizi hayo.

Katika taarifa, jeshi la Israeli lilisema limefanya "shambulio lililolenga kamanda aliyewajibika kwa shambulio hilo na mauaji ya raia wa Israeli."

Reuters