Rais wa china Xi Jinping: China yataka mzozo wa Israel na Hamas kumalizwa haraka

Rais wa china Xi Jinping: China yataka mzozo wa Israel na Hamas kumalizwa haraka

Beijing imesema iko tayari kushirikiana na serikali za Kiarabu ili kupata suluhisho la kudumu la mzozo huo.
Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba wakati wa chakula cha jioni cha mapokezi katika ukumbi kabla ya Siku ya Kitaifa ya China huko Beijing, China mnamo Septemba 28, 2023. Jade Gao / Pool kupitia Reuters / Picha ya zamani

China inataka vita kati ya Israel na Hamas kusitishwa haraka iwezekanavyo, Rais Xi Jinping alinukuliwa na vyombo vya Habari vya Serikali ya China siku ya Alhamisi.

Aidha, Beijing imeeleza kuwa iko tayari kufanya kazi na serikali za Kiarabu ili kupata suluhu la kudumu ya mzozo huo.

Xi ameongeza kuwa mapigano ni "lazima" yasitishwe haraka iwezekanavyo ili kuzuia mzozo kupanuka, au kuongezeka kwa udhibiti, vyombo vya habari vya serikali viliongeza.

Rais huyo wa China aliyasema hayo baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly, ambaye alikuwa mjumbe mwandamizi pekee kutoka Mashariki ya kati kuhudhuria mkutano wa miundombinu ya Ukanda na Barabara ya China wiki hii.

China inaunga mkono juhudi za Misri za kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikishwa Gaza, vyombo vya habari vya serikali vilimnukuu Xi akimwambia Madbouly.

Matamshi hayo ya rais wa China ni miongoni mwa matamshi ya kwanza aliyoyatoa tangu mzozo huo ulipozuka mnamo Oktoba 7, na kusababisha shambulio kubwa la kijeshi dhidi ya Gaza.

Siku ya Jumatano, Misri na Marekani zilikubaliana kuleta misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza "kwa njia endelevu" kupitia Sinai ya Misri.

Kando na hayo, Xi pia alisema China iko tayari kufanya kazi na Misri kuimarisha ushirikiano katika miundombinu, teknolojia ya kilimo na nishati mbadala, akiongeza kuwa pia atahimiza biashara zenye uwezo za Wachina kuwekeza huko.

Reuters