China imeigiza "kuifunga" Taiwan wakati wa siku ya tatu ya mazoezi ya kivita kuzunguka kisiwa hicho kinacho jitawala chenyewe, huku Marekani ikipeleka maangamizi katika maji yanayo daiwa kuwa ya Beijing ili kuonyesha nguvu.
Baada ya siku mbili za mazoezi ambayo ni pamoja na kuonyesha mashambulizi yaliyo lengwa dhidi ya Taiwan na kuzunguka kisiwa hicho, jeshi la China lilisema Jumatatu kwamba michezo ya kivita pia ni pamoja na "kuifunga".
Moja ya kombora la china ambalo pia linabeba ndege lilishiriki katika "mazoezi hayo ya kijeshi", jeshi lilisema.
China ilizindua mazoezi hayo kumjibu Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen wiki iliyopita alipokutana na spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy, mkutano ambao ulitarajiwa ungezua jibu la hasira.
Marekani, ambayo mara kwa mara iliitaka China kujizuia, siku ya Jumatatu ilituma chombo cha kuangamiza makombora cha USS Milius kupitia sehemu zinazo gombaniwa za Bahari ya China Kusini.