Ornamental chicken was the gate of livelihood / Photo: AA

Kulingana na gazeti la serikali la China Daily, jamaa huyo aliwahi kutumia tochi "kuwatisha kuku," ambapo iliripotiwa kwenye mahakama kaunti ya Hengyang.

Ripoti zinasema kwamba Gu alitumia mwangaza wa tochi, ambao ulieneza hofu miongoni mwa kundi la ndege hao. Matokeo yake, ndege hao walikusanyika pamoja kwa hofu na 540 kati yao walikandamizwa hadi kufa kutokana na kulazimishwa kwenye kona.

Aliingia shambani kinyume cha sheria mara ya pili na kusababisha vifo vya kuku 640.

Tukio hili la kushangaza lilianza Aprili mwaka jana wakati mwanamume huyo, anayefahamika kwa jina Gu, alikasirika kuwa jirani yake, Zhong, alikuwa amekata miti yake bila idhini yake.

Gu, mkazi wa Kaunti ya Hengyang katika Mkoa wa Hunan, kusini-kati mwa China, aliingia kwa siri katika shamba la kuku la Bw. Zhong mara kadhaa usiku kucha kama kulipiza kisasi. Hakusema alichokuwa akifanya akiingia shambani kisiri.

Kuku hao 1,100 waliokufa walikadiriwa kuwa na thamani ya yuan 13,840 na mamlaka ya Uchina ambayo Gu aliagizwa kulipa.

Ingawa Gu alikuwa ameeleza majuto kwa matendo yake, mahakama siku ya Jumanne iligundua kuwa hatua yake ilikuwa ya makusudi na kumhukumu kifungo cha miezi sita gerezani.

TRT Afrika na mashirika ya habari