Polisi wa Uingereza wanawashtaki watu kadhaa kwa kushambulia maandamano yanayounga mkono Palestina

Polisi wa Uingereza wanawashtaki watu kadhaa kwa kushambulia maandamano yanayounga mkono Palestina

Watu wawili kati ya watu hao wanakabiliwa na makosa ya ubaguzi wa rangi, ambayo yanahusisha kuonyesha bango la kutishia maisha na ubaguzi.
Ilikuwa ni wikendi ya tatu mfululizo ambapo London iliandaa mkutano mkubwa wa kuwaunga mkono Wapalestina. / Picha: Reuters

Polisi mjini London wamesema kuwa watu watano wamefunguliwa mashtaka baada ya kukamatwa wakati wa maandamano ya wafuasi wa Palestina siku moja kabla, ambayo yalishuhudia makumi ya maelfu wakiandamana kwa ajili ya usitishaji mapigano huko Gaza.

Polisi wa Metropolitan waliwakamata watu tisa siku ya Jumapili - wawili kwa tuhuma za kuwashambulia maafisa wa polisi na saba kwa makosa ya utaratibu wa umma.

Watu wengine wawili walikamatwa Jumapili asubuhi, wakishukiwa kuchochea chuki ya rangi kufuatia tukio katika Trafalgar Square Jumamosi jioni, idara y apolisi ya Met ilisema katika taarifa.

Miongoni mwa washtakiwa watano, wenye umri wa kati ya miaka 16 na 51, wawili walishtakiwa kwa makosa ya ubaguzi wa rangi, ikiwa ni pamoja na kuonyesha bango "linalotishia maisha na ubaguzi wa rangi".

Wengine walishtakiwa kwa kumrushia mkebe wa bia mandamanaji na kuwashambulia kwa maneno na kimwili maafisa wa polisi.

'Maandamano kwa ajili ya Palestina'

Takriban watu 100,000 walijiunga na "Machi kwa Palestina" huko London Jumamosi kulingana na vyombo vya habari vya Uingereza, ambavyo pia viliripoti ugomvi na polisi.

Ilikuwa ni wikendi ya tatu mfululizo ambapo London iliandaa mkutano mkubwa wa kuwaunga mkono Wapalestina tangu Oktoba 7, wakati Israel ilipoanza mashambulizi makali ya mabomu huko Gaza kufuatia shambulio la kushtukiza la kundi la Palestina Hamas.

Idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza imeongezeka hadi 8,005, wakiwemo watoto 3,342, wanawake 2,062 na wazee 460, kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina katika eneo lililozingirwa.

Waandalizi walidai kuwa watu 500,000 walishiriki Jumamosi hii, ikilinganishwa na 300,000 wiki iliyopita.

Polisi wa Metropolitan wa London walituma zaidi ya maafisa 1,000 kushika doria kwenye maandamano hayo.

TRT World