Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis amewataka waumini wote kufunga na kuombea amani ya ulimwengu siku ya Oktoba 7, wakati dunia ikikumbuka mwaka mmoja toka kuanza kwa mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza.
“Kadiri pepo za vita na machafuko zinavyoendelea kuiharibu dunia na mataifa mengine, jumuiya ya Wakristo inakumbushwa kusali na kutafakari amani ya dunia,” Papa Francis alisema.
Kulingana na Papa Francis, mgogoro huo, sio tu kwamba umeleta "maafa ya kibinadamu, lakini pia umechochea mabadiliko tofauti ya kisiasa ulimwenguni.”
Huku ikiendelea kukaidi azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Israeli imeendelea kuishambulia Gaza tangu Oktoba 7, 2023.
Mashambulizi hayo, yaliyodumu kwa mwaka mmoja sasa, yameua watu takribani 41,900, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi wengine zaidi ya 97,000, kulingana na mamlaka za afya.
Israeli pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, kufuatia vitendo vyake dhidi ya Gaza.