Netanyahu, "hana imani na majaji, akihofia kwamba watalipiza kisasi dhidi yake kwa sababu ya mageuzi ya kisheria," ambayo yalisababisha maandamano ya miezi kadhaa nchini Israeli. /Picha: AP

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anataka kuzuia uteuzi wa wajumbe wa tume ya uchunguzi kuhusu shambulio la Oktoba 7 lililotekelezwa na Hamas, gazeti la Haaretz lilisema.

"Netanyahu anataka kuondoa mamlaka ya kuteua wajumbe wa kamati kutoka kwa rais wa Mahakama ya Juu ya Israeli," Haaretz alisema Jumapili.

"Netanyahu hataki jaji kuongoza kamati ya uchunguzi kuhusu matukio ya Oktoba 7," iliongeza.

Mshauri wa usalama wa taifa, wa Netanyahu Tzachi Hanegbi, alisema mapema Jumapili kwamba kamati ya uchunguzi italenga kumaliza utawala wa mrengo wa kulia nchini Israel, kulingana na gazeti la Yedioth Ahronoth.

Gazeti hilo, likimnukuu afisa katika ofisi ya Netanyahu, lilisema waziri mkuu huyo wa Israeli "hana imani na majaji, akihofia kwamba watalipiza kisasi dhidi yake kwa sababu ya mageuzi ya kisheria," ambayo yalisababisha maandamano ya miezi kadhaa nchini Israeli.

Tume ya uchunguzi ya serikali

Mnamo Aprili 26, Waziri wa Vita wa Israel Benny Gantz, alipendekeza kuundwa kwa tume ya serikali ya uchunguzi kuhusu matukio ya Oktoba 7 na vita vilivyofuata vya Israeli dhidi ya Gaza.

Zaidi ya Wapalestina 36,400 wameuawa huko Gaza kufuatia mashambulizi mbaya ya Israeli huko Gaza tangu Oktoba 7, wakidai kulipiza shambulio la Hamas.

Wengi wa waliouawa ni wanawake na watoto, huku wengine zaidi ya 82,600 wakijeruhiwa, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.

Maeneo makubwa ya Gaza yamekua magofu huku kizuizi cha Israeli kikisabisha uhaba wa chakula, maji safi, na dawa.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ambayo uamuzi wake wa hivi karibuni uliiamuru Tel Aviv kusitisha mara moja operesheni yake huko Rafah, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni 1 walikuwa wamekimbilia kutafuta hifadhi kutokana na vita vya mauaji ya halaiki.

TRT World