Na Ian Proud
Mwezi uliopita wa 2024 ulishuhudia maandamano makubwa ya raia katika mji mkuu wa Georgia, Tbilisi na utangazaji wa vyombo vya habari ambao haujawahi kufanywa juu ya kile kilichotangazwa kama "maandamano ya kuunga mkono Ulaya" na Magharibi.
Muda ulipozidi kuyoyoma wa muhula wa miaka sita wa Salome Zourabichvili kama rais wa taifa hilo dogo linalozunguka Ulaya na Asia, wafafanuzi wa nchi za Magharibi walizidisha shinikizo la kumtangaza rais anayekuja Mikheil Kavelashvili kama asiyekuwa wa sheria.
Zourabichvili alisita kuachia ngazi licha ya kuwa chama cha Georgian Dream kimeshinda uchaguzi.
Marekani na Uingereza zilitekeleza wajibu wao kwa kuwawekea vikwazo maafisa wa serikali ya Georgia Dream.
Tumetarajia kuwepo kwa uwezekano wa mapinduzi kama yale ya Maidan. Mwishowe, Kavelashvili aliapishwa bila ya chamgamoto, na vyombo vya habari vya kigeni vikakubali matokeo.
Marekebisho ya Katiba
Kurudi nyuma hadi Desemba 2018, kuapishwa kwa Zourabichvili kama rais wa mwisho wa Georgia aliyechaguliwa moja kwa moja kuliambatana na kuanza kutumika kwa katiba mpya ya Georgia.
Mabadiliko hayo yalitokana na wasiwasi kuhusu ufisadi katika siasa za uchaguzi za Georgia tangu uhuru mwaka 1991. Katiba mpya imeamuru kwamba rais achukue madaraka yasiyokuwa na mamlaka makubwa, lakini kutoka 2024, achaguliwe kwa njia isiyo ya moja kwa moja na bunge. Mfumo kama huo unatumika katika nchi kadhaa za EU, pamoja na Ujerumani.
Kwa hivyo, mabadiliko ya kikatiba ya Georgia kwa mfumo wa demokrasia ya bunge hayakuwa kinyume na kile kinachotokea katika nchi nyingi za Ulaya. Wala Zourabichvili hakuwa amepinga mabadiliko haya ya mipangilio ya kikatiba kabla ya majira ya kuchipua ya 2024.
Katiba mpya pia ilijumuisha vipengele vya kuanzisha uwakilishi kamili wa sawia kwenye uchaguzi na upigaji kura wa kielektroniki, mambo ambayo yalisifiwa sana wakati huo na makundi ya upinzani.
Manmo 2024, chama cha Georgia Dream kilishinda uchaguzi wa bunge wa Oktoba 26 chini ya mfumo huu kwa asilimia 54 ya kura, huku vyama vinne vya upinzani vilivyogawanyika kwa pamoja vilipata asilimia 37.
Wakati ujumbe wa ufuatiliaji wa OSCE ulipata dosari katika vipengele kadhaa vya mchakato wa uchaguzi, hata hivyo wameripoti kwamba uchaguzi ulipangwa vyema.
Walakini, Zourabichvili ameongoza kampeni ya kuhimiza kutotambuliwa kwa matokeo, na Uingereza na Marekani, haswa, zimechukua nafasi katika kumuunga mkono.
Mwakilishi Joe Wilson, Mwenyekiti wa Tume ya Usalama na Ushirikiano ya Marekani ya Helsinki barani Ulaya inayoongozwa na Marekani, alitoa wito kwa mitandao ya kijamii kutoitambua "Ndoto ya Kijojia", akikusudia kukikejeli chama cha Georgia Dream.
Tume ya Helsinki pia ilitoa wito wa vikwazo dhidi ya maafisa wa Georgia, na mnamo Desemba 19, Marekani na Uingereza ziliweka vikwazo vya adhabu kwa maafisa watano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Georgia, ikiwa ni pamoja na waziri.
Mnamo Desemba 27, Marekani pia ilimuwekea vikwazo kiongozi wa Georgia Dream, Bidzina Ivanishvili, kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, "kwa kudhoofisha mustakabali wa kidemokrasia na Euro-Atlantic wa Georgia".
Umoja wa Ulaya ulibatilisha usafiri bila viza kwa wanadiplomasia na maafisa wa Georgia.
Maandamano ya awali huko Tbilisi kufuatia uchaguzi wa Oktoba 26 yalikuwa ya vurugu, na hivyo kuzua hofu kwamba matukio ya Tbilisi yanaweza kuakisi vuguvugu la maandamano ya Maiden huko Kiev, ambayo yaliishia kwa mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo wa Ukraine, Viktor Yanukovych mnamo Februari 2014.
Tofauti ya Tbilisi ilikuwa kwamba vuguvugu la maandamano lilikuwa na lengo la kuunda aina ya kipekee ya mapinduzi ambayo rais anayehudumu wa Georgia angebaki madarakani kinyume na katiba.
Katika suala hilo, Zourabichvili alikuwa mfano mbaya zaidi wa mbabe wa kisiasa anayejitafutia maslahi yake mwenyewe, akitumia kisingizio cha madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi kung'ang'ania madaraka ya kisiasa.
Walakini, vuguvugu la maandamano ya baada ya uchaguzi, likiwa bado limeenea, lilipungua kwa mikusanyiko ya amani na maandamano ambayo polisi wa Georgia walionekana kushughulikia kwa utulivu.
Majaribio ya Ulaya na Marekani ya kufadhili kupinduliwa kwa serikali halali huko Tbilisi yalishindikana, na sasa tuko katika hali mbaya wakati serikali za Magharibi zinaamua iwapo na jinsi ya kurejesha uhusiano.
Kwa nini Uturuki ni muhimu
Matukio ya hivi majuzi yanatoa uthibitisho wa kutosha kwamba badala ya kukabiliana na chaguo la Euro-Atlantic, Georgia inapaswa kuzingatia ushirikiano wake wa kudumu karibu na nyumbani, na Uturuki.
Kama vile Georgia, njia yenye matatizo ya Uturuki kuelekea uanachama wa EU, kwa sasa, imezidi kuwa ngumu.
Ingawa mchakato wa kujiunga unatambuliwa rasmi kuwa umeganda, binafsi nina shaka kuwa Uturuki itaweza kujiunga na EU kama mshirika kamili na sawa kwa nchi nyingine wanachama.
Kimsingi, sijawahi kuamini kwamba jumuiya hiyo yenye Wakristo wengi ingetaka taifa la Waislamu wenye nguvu kama Uturuki kujiunga nao , na hivyo, kuwa mwanachama mkubwa zaidi wa Umoja wa Ulaya kwa idadi ya watu.
Gharama ya mshikamano wa EU kwa kuruhusu Uturuki kujiunga inaleta changamoto kubwa zaidi kuliko gharama ya kufyonza Ukraine, ambayo ingevunja bajeti ya EU.
Kuhusu Georgia, maslahi ya Umoja wa Ulaya yanaonekana zaidi kuwa juu ya ujenzi wa taifa wa kawaida, ambao chama cha Georgia Dream kinaona wazi kama uingiliaji wa nje.
Ukweli wa wazi ni kama nilivyoandika hapo awali kwamba Georgia imepoteza kiuchumi kufuatia utekelezaji wake wa makubaliano ya kina ya biashara huria na EU mnamo 2016.
Kama ilivyo kwa Ukraine, EU inataka nchi mfano wa Georgia ambayo inaweza kushindwa kutekeleza masharti, Georgia inataka manufaa ya kiuchumi ambayo Ulaya inaweza kuwa haitaki au haiwezi kutoa.
Kadhalika, njia ya 'Euro-Atlantic' ambayo wabunge wa Marekani wanazungumzia - kanuni ya uanachama wa NATO wa siku zijazo - pia ni chaguo lisilowezekana kwa Georgia.
Baada ya kuingizwa kwenye vita vya uharibifu na Urusi mnamo 2008 juu ya matarajio yake ya kujiunga na NATO wakati huo, itakuwa upumbavu mkubwa kwa viongozi wa Georgia kufufua wazo hilo sasa.
Hiyo haifanyi Georgia kuwa rafiki wa Urusi. Georgia bado haina uhusiano wa kidiplomasia na Urusi, na chama cha Georgia Dream bado kinataka kurudisha tena mikoa inayojitenga ya Abkhazia na Ossetia Kusini siku moja.
Uturuki imechukua msimamo sawia na kuwajibika kuhusu demokrasia ya Georgia katika kipindi cha baada ya uchaguzi.
Kwa ukaribu wao, Uturuki na Georgia zimejenga uhusiano wa kimkakati wa kibiashara na uwekezaji.
Wakati uhusiano wa kibiashara unaipa ubora Uturuki kutokana na ukubwa wake, ikiwa na ziada ya dola bilioni 2 kwa mwaka, hii inakabiliwa kwa sehemu na jukumu la Ankara kama mwekezaji mkubwa wa kigeni wa moja kwa moja nchini Georgia.
Ushirikiano huu ni muhimu wakati ambapo Uturuki na nchi jirani ya Caucasus Kusini ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwa usalama wa nishati wa Uropa kufuatia Urusi kujitenga zaidi na masoko ya nishati ya EU.
Ukanda wa kusini wa gesi - unaopitia Azarbaijani, Georgia na Uturuki - umeongezeka kwa umuhimu kufuatia uamuzi wa Ukraine wa kukata upitishaji wote wa gesi ya bomba kutoka Urusi kwenda Ulaya kutoka Januari 1.
Uturuki na Georgia wamechagua kutozingatia vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi, kutokana na madhara ya kiuchumi ambayo yatawasababishia kwa kufanya hivyo.
Ingawa ni nchi muhimu ya NATO, Uturuki imekuwa ikitafuta suluhu la mazungumzo nchini Ukrainia kupitia mazungumzo ya amani ya Istanbul Februari 2022 au kupitia nafasi yake kuu katika kuwezesha mpango wa Nafaka ya Bahari Nyeusi.
Chama cha Georgia Dream kimeelezea wasiwasi wake kuhusu vita nchini Ukraine, baada ya kuathiriwa na idadi kubwa ya watu, ikilinganishwa na idadi ndogo ya wananchi, inayo athiriwa kwa kufurika kwa wanaokimbia kuhudumia jeshi kutoka Urusi na Ukraine na wahamaji wa wanaotafuta maisha mazuri tangu kuanza kwa mzozo huo.
Kwa hivyo, katika safu kubwa ya maswala ya kiuchumi, kisiasa na usalama, Uturuki na Georgia zinafurahia kiwango cha juu cha usawa kilichojengwa juu ya misingi ya uhusiano thabiti wa kidiplomasia.
Serikali ya Georgia Dream inapoangazia upya kurekebisha na kujenga upya uchumi wake, Uturuki itaendelea kuwa mshirika thabiti na anayetegemewa kuliko Umoja wa Ulaya au Marekani.
Mwandishi, Ian Proud ni mwanadiplomasia wa zamani wa Uingereza na mwandishi wa kitabu: "A Misfit in Moscow: How British Diplomasy in Russia Failed".
Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayaakisi maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.