Israel ililenga kikundi cha waandishi wa habari katika eneo la Gaza, Ijumaa mchana, na kujeruhi wafanyakazi wawili wa TRT Arabi, ambapo mmoja alipoteza mguu wake (Picha: AA) 

Waandishi wawili wa habari wa TRT Arabi wamejeruhiwa katika shambulizi jipya la Israel siku ya Ijumaa mchana katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Gaza. Mpiga picha Sami Shehadeh alijeruhiwa vibaya huku madaktari wakilazimika kuukata mguu wake wa kulia.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Jeshi la Israel lililenga kundi la waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na timu ya Kiarabu ya TRT, waliokuwa wakiripoti kutoka kambi ya wakimbizi ya Nuseirat. Baadhi ya waandishi wa habari walijeruhiwa baada ya kusmabuliwa na kifaru cha Israel.

Mwakilishi wa TRT Arabi Sami Berhum na waandishi wengine pia walijeruhiwa kwenye tukio hilo.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Gaza, waandishi wa habari wasiopungua 140 wamepoteza maisha katika mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Siku ya jana, Jeshi la Israel lilitangaza kuanzisha "operesheni ya kushtukiza" katikati mwa Gaza, na kusababisha mauaji ya Wapalestina wengi.

Mkurugenzi Mkuu wa TRT, Zahid Sobaci alilaani shambulio hilo, na kulielezea kama "ukatili" usio na "kikomo cha maadili, kisheria au kibinadamu."

Reuters