Na Richard Falk
Israeli katika mwaka mmoja tangu baada ya mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas tarehe 7 Oktoba imedai kuwa inachochewa na malengo ya kupambana na ugaidi ili kuwaangamiza Hamas, na hivi karibuni zaidi, kuiangamiza Hezbollah kama adui wa kuaminika, na katika mchakato huo kudhoofisha hasimu wake Irani anayo iogopa.
Madhumuni yake ya ziada yamekuwa kuwafanya Hamas, Hezbollah, na Houthis wa Yemen kama vibaraka wa adui mkubwa wa Iran, ambayo inashutumiwa kuwa mwezeshaji mkuu wa "ugaidi dhidi ya Israeli" katika Mashariki ya Kati, muungano unaoelezewa kwa dharau huko Magharibi kama "mhimili wa upinzani."
Kuharibu zaidi katika siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kutisha ya Oktoba 7, ni uvamizi kama wa Gaza uliofanywa na Israeli katika wiki za hivi karibuni dhidi ya Hezbollah kusini mwa Lebanon.
Ni mashambulizi mapya na unyanyasaji yaliyotekelzwa na Israeli kupitia vifaa vya mawasiliano vya 'pager' yaliyofuatiwa siku chache baadaye na mauaji ya kiongozi wa muda mrefu wa Hezbollah, Hassan Nasrallah mnamo Septemba 27.
Na hii ilikuwa ni mwaka mmoja baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuzungumzia ulimwengu "kutozuilika huku mivutano ya kijiografia ikiongezeka."
Huku kukiwa na wasiwasi huu wa ripoti za kila siku za ukatili na mateso ya raia kwa muda mrefu, swali linaanza kuulizwa kutokana na kukithiri kwa ghasia za Israeli pamoja na kukataa kwa ukaidi kukubali uungwaji mkono wa karibu wote wa makubaliano ya kusitisha mapigano/mabadilishano ya wafungwa huko Gaza: Je, ni lengo gani la kimkakati la Israeli ambalo lina thamani ya kujitolea kiasi hiki katika sifa yake ya kimataifa kama nchi yenye nguvu na ya kisheria?
Na kinachonyemelea nyuma ya swali hili la kuhuzunisha ni swali linalohusiana na wasiwasi: Je, Israeli ina mwisho ambao unaweza kuthibitisha, angalau machoni pake, kujitolea huku ni pamoja na kukubalika kwa unyanyapaa wa jinai wa madai ya kuaminika ya ubaguzi wa rangi na mauaji ya kimbari, na uhalifu dhidi ya ubinadamu?
Mpango wa mwisho wa Natenyahu
Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alionekana mjini New York na kutoa hotuba ya ajabu mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililo susiwa na wajumbe wengi, akieleza maono ya Israeli ya amani.
Katika shambulio la kujenga mwelekeo wenye kupotosha, aliutaja Umoja wa Mataifa kama "lindi la nyongo dhidi ya Wayahudi," ambapo tuhuma zozote dhidi ya Israeli, hata kama ni potofu, zinaweza kupata "uwingi wa moja kwa moja" dhidi ya taifa pekee lenye Wayahudi wengi duniani katika ''jamii hii inayokataa ukweli ulio wazi' akimanisha UN.
Ilikuwa katika hali hii ya kutatanisha ambapo Netanyahu alichagua kutangaza maono yake makubwa ya Israeli ambao unadai kuleta amani na ustawi katika eneo hilo.
Kile ambacho Netanyahu aliwasilisha kwenye baraza liliokuwa tupu la Umoja wa Mataifa (kwa sababu wajumbe wengi waliondoka wakisusia hotuba yake) kilikuwa kifurushi cha siasa za kijiografia kilichounganishwa pamoja na usemi wa "baraka za amani."
Kimsingi ilikuwa ni manifesto ambayo hatua ya kwanza ilihusisha kuangamizwa kwa maadui wa Israeli, washirika wa Iran.
Ilipaswa kufuatiwa na hatua ya pili ya "makubaliano ya kihistoria ya amani na Saudi Arabia" yaliyowasilishwa kama mwendelezo wa ajabu wa Makubaliano ya Abraham yaliyofikiwa katika kipindi cha mwisho cha urais wa Donald Trump miaka minne iliyopita.
Maneno haya yanayotangaza "Mashariki mpya ya Kati" yalisisitizwa na Netanyahu, ambaye akieleza, " baraka za amani ambazo zitakuja na nchi ya Saudi Arabia."
Mbali na wale ambao walitaka kudanganywa na mchezo kama huo uliopangwa, watu wengi walioarifiwa waligundua kuwa ulikuwa ni mfano mbaya wa propaganda za serikali.
Netanyahu alionyesha ramani ya Mashariki yake mpya ya Kati ambayo haitoi uwepo wa taifa la Palestina, ingawa Saudi Arabia ilikuwa imesisitiza kwamba haitaanzisha amani na Israeli hadi taifa la Palestina litakapokuwepo.
Muungano wa Netanyahu na vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia unaoongozwa na watu wenye misimamo mikali kama vile Waziri wa Usalama wa Kitaifa Itamar Ben-Gvir na Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich ungesambaratika mara tu dhamira yoyote ya kweli kwa utawala wa Palestina ilipoidhinishwa rasmi.
Haiwezekani kuamini kwamba Netanyahu hakufahamu kikwazo hiki, na hivyo inaonekana kuwa haiwezekani, kuiweka kwa upole, kwamba alitarajia shauku yoyote hata huko Washington kwa maono yake ya mwisho wa kujenga amani.
Kuchunguza mpango wa mwisho wa kweli wa Israeli
Chini ya wazo la mahusiano ya umma la mpango wa mwisho wa Israeli kuna ukweli wa kutisha.
Hata kabla ya serikali ya Netanyahu kuchukua hatamu mwanzoni mwa 2023, ilikuwa dhahiri kwamba ajenda ya kisiasa ya Israeli ilikuwa na mwisho usiojulikana ambao ungekamilisha Mradi wa Kizayuni baada ya karne ya juhudi za ukoloni walowezi.
Hili lilinidhihirika kwa mara ya kwanza wakati serikali ya Israeli ilipoanzisha Sheria ya Msingi ya kikatiba mwaka wa 2018. Pamoja nayo, haki za Kiyahudi za kutawala kuliko zote ziliandikwa katika sheria za Israeli kama zinazotoa haki ya kujitawala pekee kwa Wayahudi, ikiweka Kiebrania kama lugha rasmi pekee ya Israeli, na kupanua makazi huru ya Israeli kwa makazi yanayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi.
Ilikuwa ni hatua hii ya kisheria ya Knesset ambayo ilithibitisha mwisho wa Israeli wa suluhisho la taifa moja linalojulikana sana kama "Israeli Kubwa," fomula ya kupanua mamlaka ya Israeli juu ya Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki kwa kukiuka sheria za kimataifa na makubaliano ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na nchi za Magharibi.
Sheria kama hiyo ya Msingi haiwezi kubadilishwa kwa hatua ya kawaida ya kisheria, lakini tu na Sheria ya Msingi iliyobatilishwa na sheria mbadala.
Muungano wa Netanyahu ulipochukua mamlaka, kulikuwa na ishara za uchochezi kwamba Sheria hii ya Msingi ya 2018 ingeharakishwa kwa lazima kama kipaumbele nambari moja cha Israeli.
Hapo awali ilionyeshwa na mwanga usio rasmi, lakini usio na shaka, wa ghasia za walowezi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na ujumbe ulioelezwa mara kwa mara kwa wakazi wa Palestina: "ondoka au tutakuua."
Mnamo Septemba 2023, hotuba ya Netanyahu ya Umoja wa Mataifa iliyoonyesha ramani ya eneo lisilo na Palestina iliimarishwa na juhudi kali za kidiplomasia kupata uhalalishaji wa Kiabrahamu na baadhi ya mataifa ya Kiarabu, dalili zaidi za kuanzisha kile kinachojulikana kama "Israeli Kubwa".
Vitendo hivi pamoja na chokochoko katika boma la Msikiti wa Al Aqsa vilisaidia kuweka mazingira ya shambulio lililoongozwa na Hamas mnamo Oktoba 7, tukio lenyewe ambalo sasa limegubikwa na utata ambalo linaweza kuondolewa tu na uchunguzi wa kimataifa.
Makosa ya pande zote mbili
Ulimwengu mwanzoni ulikubali kwa kiasi kikubwa, au angalau ulivumilia toleo la Israeli la Oktoba 7, ikiwa ni pamoja na mantiki yake ya kulipiza kisasi kutokana na kisingizio cha sheria ya kimataifa kama utekelezaji wa "haki ya kujilinda".
Kadiri habari zaidi zilivyopatikana, uhalalishaji wa asili wa Israeli kwa majibu yake hadi Oktoba 7 ukawa wa shida. Ilibainika kuwa uongozi wa Netanyahu ulikuwa umepokea maonyo kadhaa ya kuaminika ya shambulio la Hamas lililokaribia.
Baada ya miezi kadhaa ya mafunzo, inaonekana ni jambo lisiloaminika kwamba uwezo wa uangalizi wa kiwango cha kimataifa wa Israeli haukutahadharishwa, na ukubwa na uzito wa mara moja wa jibu hilo uliibua shaka kwamba Israeli ilikuwa inatafuta kisingizio cha kushawishi kuwahamisha Wapalestina kutoka Gaza na kufuatiwa na Ukingo wa Magharibi inayokaliwa kwa mabavu.
Hii ilionekana kuwa utangulizi wa kuaminika wa kuanzishwa rasmi kwa "Israeli Kubwa", na kupatikana kwa mpango wa mwisho wa kweli wa Israeli.
Kwa kutazama nyuma, Hamas na Israeli wanaonekana kuwa wamekosea sana. Israeli inaonekana kuzingatia ghasia za mauaji ya kimbari, zitakazo sababisha kujisalimisha kisiasa au uhamishaji wa mpaka, na wimbi jipya la wakimbizi wa Kipalestina.
Israeli ilipuuza uhusiano wa Wapalestina katika ardhi hiyo, hata katika hali ya uharibifu kamili. Pia kumekuwa na ongezeko la maoni ya watu wenye uhasama duniani kote kuhusu ghasia za Israeli, kutokana na ukatili unaofanywa na mateka walionaswa katika shambulio hilo lililoongozwa na Hamas.
Kwa upande wake, Hamas ilidharau ukali wa jibu la Israeli kwa sababu ilifikiria shambulio lake katika hali ya kawaida ya uwanja wa vita utapata majibu ya kawaida, hawakudhania utakuwa mpango wa mwisho wa Israeli.
Madai yasiyo kweli ya Israeli ya ushindi yanaonyesha kuwa muungano wa Netanyahu umejitolea kama vile awali kwenye mpango wa mwisho wa "Israeli Kubwa", huku upanuzi wa eneo la mapigano na kujumuisha Lebanon inaonekana kuifanya iwe na nguvu zaidi.
Baada ya kuvumilia mengi, ni vigumu kufikiria kuwa Wapalestina watakubali mpango wa mwisho wa Israeli hata baada ya mashambulizi na mauaji ya halaiki ya Israeli, ikiwa mpango huo haujumuishi kuanzishwa kwa mustakabali mzuri wa kisiasa wa Palestina. Hili linaweza kuwa taifa linalofaa la Palestina au shirikisho jipya la serikali moja linaloaminika kwa msingi wa usawa kamili kati ya watu hawa wawili.
Kwa kumalizia, hali za kisiasa hazipo kwa sasa kwa mchezo wa mwisho ambao unaweza kukidhi matarajio ya chini ya watu wote wawili.
Mwandishi, Richard Falk ni Profesa wa International Law Emeritus, Chuo Kikuu cha Princeton, Ripota Maalum wa zamani wa Umoja wa Mataifa kwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na mwandishi mwenza wa "Liberating the United Nations: Realism with Hope" (2024). iliyochapishwa hivi karibuni. Ameteuliwa kwa Tuzo ya Amani ya Nobel mara kadhaa tangu 2008.
Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayawakilishi lazima maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.