Moshi wa hospitali ya Gaza iliyopigwa bomu utaifunika Israel, Rais wa Iran Raisi asema

Moshi wa hospitali ya Gaza iliyopigwa bomu utaifunika Israel, Rais wa Iran Raisi asema

Rais wa iran ametangaza jumatano kuwa siku ya 'maombolezo ya umma'
Rais wa Iran Ibrahim Raisi ametangaza Jumatano kuwa siku yamaombolezo ya kitaifa /Picha AA

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amelaani shambulizi la siku ya jumanne dhidi ya Hospitali ya Baptist ulioko Ukanda wa Gaza, akionya kuwa moto wake "hivi karibuni utaikumba" Israel.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X mwishoni mwa jumanne, Raisi alisema "moto wa mabomu Ya Marekani na Israeli" yaliyotupwa kwenye hospitali ya Gaza "hivi karibuni yatawafunika Wazayuni."

"Ukimya wa mtu yeyote huru hauruhusiwi mbele ya uhalifu huu wa kivita", alisema, huku akitangaza Jumatano kuwa siku ya "maombolezo ya umma" nchini kote.

Zaidi ya watu 500 waliuawa katika shambulio la Anga la Israel dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli Baptist mwishoni mwa jumanne, msemaji wa Wizara ya Afya Ashraf Al-Qudra aliiambia Anadolu.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha miili ikitawanyika katika uwanja wa hospitali.

Shambulio hilo la anga lilikuja siku ya 11 ya mzozo kati ya Israel na Hamas, na kuongezeka kwa wito wa kimataifa ya makundi yasiyo ya kiserikali na viongozi wa dunia wakisema kampeni ya mabomu ya Israeli kwenye eneo lililozingirwa ikiwa ni pamoja na vituo vya huduma za afya, nyumba, na nyumba za ibada, inakiuka sheria za kimataifa na inaweza kuwa uhalifu wa vita.

Awali, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani pia alilaani shambulio la hospitali, akiitaja kama "uhalifu wa kikatili wa vita" na "mauaji ya kimbari."

"Utawala wa kizayuni, katika mwendelezo wa uhalifu wake wa aibu dhidi ya Watu wa Palestina, kwa kufanya uhalifu huu mbaya na wa kutisha, umeonyesha tena unyama na ukatili wake kwa kila mtu," alisema.

Wakati huo huo, maelfu ya watu walikusanyika Jumanne usiku katika uwanja wa Palestina ulioko katikati ya mji wa Tehran ili kuwaunga mkono watu wa Palestina na kulaani shambulio hilo dhidi ya hospitali ya Gaza.
AA