Mashambulizi ya Israel yamezima viwanja viwili vikuu vya ndege vya taifa la Syria lililokumbwa na vita, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti, vikinukuu chanzo cha kijeshi, huku wizara ya uchukuzi ikisema safari za ndege zilielekezwa uwanja wa Latakia.
Hii ni mara ya pili kwa mashambulizi ya wakati mmoja kukumba viwanja hivyo siku ya Jumapili tangu mzozo wa mwezi huu kati ya Israel na Hamas kuanza.
"Mnamo saa 5:25 asubuhi (0225 GMT), adui Israel walifanya shambulio la angani likilenga viwanja vya ndege vya Damascus na Aleppo, na kusababisha kifo cha mfanyakazi wa kawaida katika uwanja wa ndege wa Damascus na kumjeruhi mwingine," chanzo cha kijeshi kilisema katika taarifa hiyo iliyobebwa na shirika la habari la serikali SANA.
Katika taarifa tofauti kutoka kwa Kurugenzi ya Hali ya Hewa, wafanyikazi wawili waliuawa katika shambulio hilo.
"Uharibifu wa nyenzo kwenye barabara za ndege ulivifanya visiweze kutumia ," taarifa hiyo iliongeza. Wizara ya uchukuzi ilisema safari za ndege zilielekezwa kwenye uwanja wa ndege wa Latakia.
Chanzo cha kijeshi kilisema mashambulizi hayo ya "wakati mmoja" yalikuja "kutoka upande wa Bahari ya Mediterania magharibi mwa Latakia na kutoka upande wa Golan ya Syria inayokaliwa", kulingana na taarifa hiyo.
Mashambulio ya anga yanayoendelezwa na Israel
Mnamo Oktoba 12, shambulio la wakati mmoja ulifanya viwanja vya ndege vya Damascus na Aleppo kukosa huduma, Syria ilisema wakati huo.
Wikiendi iliyopita, mashambulizi ya Israel yalilenga uwanja wa ndege wa Aleppo, na kujeruhi watu watano, uchunguzi wa vita uliripoti, pia kuufanya ushindwe kutoa huduma, kulingana na mamlaka.
Wakati wa zaidi ya muongo mmoja wa vita nchini Syria, Israel imeanzisha mamia ya mashambulizi ya angani dhidi ya jirani yake wa kaskazini, hasa yakilenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa Hezbollah wa Lebanon pamoja na maeneo ya jeshi la Syria.