Chuo Kikuu cha Columbia kimefutilia mbali masomo na makumi ya waandamanaji wengine walikamatwa katika Chuo Kikuu cha Yale na New York, huku milango ya Harvard Yard ikifungwa na baadhi ya vyuo vikuu vya kifahari vya Marekani vikijaribu kudhibiti kuenea mvutano wa vyuo vikuu kuhusu vita vya Israel huko Gaza.
Matukio mbali mbali ya Jumatatu yalifuatia kukamatwa kwa zaidi ya waandamanaji 100 wiki jana, wanaounga mkono Palestina ambao walikuwa wamepiga kambi Columbia.
Mbali na maandamano katika shule za Ivy League, wafuasi wengine wa Palestina wamekuja kwenye vyuo vikuu vingine, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts, Chuo Kikuu cha New York, na Chuo Kikuu cha Michigan.
Maandamano hayo yamewapiganisha vichwa wanafunzi wao kwa wao, huku wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina wakitaka shule zao kulaani uvamizi wa Israel Gaza na kususia makampuni yanayoiuzia Israel silaha.
Baadhi ya wanafunzi wa Kiyahudi, wakati huo huo, wanasema ukosoaji mwingi wa Israeli unawafanya wahisi hawako salama.
'Ushirikiano katika mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza'
Taharuki iliendelea kupanda siku ya Jumatatu huko Columbia katika Jiji la New York, ambapo milango ya chuo hicho ilikuwa imefungwa kwa mtu yeyote asiye na kitambulisho cha shule na ambapo maandamano yalizuka katika chuo kikuu na nje.
Mwanamke mmoja ndani ya lango la chuo aliongoza waandamanaji zaidi ya 20 wakisema kwa sauti, "Kutoka mtoni hadi baharini, Palestina itakuwa huru!" Wakati huo huo, kikundi kidogo cha waandamanaji wanaounga mkono Israeli waliandamana karibu na eneo hilo.
Siku ya Jumatatu Rais wa Chuo Kikuu cha Columbia Nemat Shafik alisema katika ujumbe kwa jumuiya ya shule kwamba "amehuzunishwa sana" na kile kilichokuwa kikitokea chuoni.
Maandamano yamekumba vyuo vingi vya Marekani tangu Israel ilipovamia Gaza.
Prahlad Iyengar, mwanafunzi aliyehitimu MIT anayesoma uhandisi wa umeme, alikuwa kati ya wanafunzi zaidi ya 20 ambao waliweka kambi ya hema kwenye chuo cha shule ya Cambridge, Massachusetts, Jumapili jioni. Wanatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na wanapinga kile wanachoelezea kama "ushirikiano wa MIT katika mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza," alisema.
"MIT haijatoa hata wito wa kusitishwa kwa mapigano, na sisi tunataka watoe wito wa kusitishwa vita," Iyengar alisema.
Pia alisema MIT imekuwa ikituma sheria za kutatanisha kuhusu maandamano.
"Tuko hapa ili kuonyesha kwamba tuna haki ya kuandamana. Na kuandamana ni sehemu muhimu ya kuishi katika chuo kikuu," Iyengar alisema.
Makubaliano kunaendelea
Matukio ya hivi punde yalikuja kabla ya kuanza kwa likizo ya Kiyahudi ya Pasaka.
Kambi ya waandamanaji iliibuka huko Columbia siku ya Jumatano, siku hiyo hiyo ambayo Shafik alikosolewa katika kikao cha bunge kutoka kwa Republican ambao walisema hakufanya vya kutosha kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi. Marais wengine wawili wa Ivy League walijiuzulu miezi kadhaa iliyopita kufuatia ushuhuda uliokosolewa pakubwa waliotoa kwa kamati hiyo hiyo.
Katika taarifa yake Jumatatu, Shafik alisema mzozo wa Mashariki ya Kati ni mbaya na kwamba anaelewa kuwa wengi wanapitia dhiki kubwa ya kimaadili.
Wanafunzi kadhaa wa Columbia na Chuo cha Barnard, walisema walisimamishwa kwa kushiriki katika maandamano ya wiki iliyopita, akiwemo mwanafunzi wa Barnard Isra Hirsi, bintiye Mwakilishi wa Kidemokrasia wa Marekani Ilhan Omar.
Huko Yale, maafisa wa polisi waliwakamata waandamanaji wapatao 45 na kuwafungulia mashtaka ya uvunjaji sheria, alisema Afisa Christian Bruckhart, msemaji wa polisi wa New Haven.
Waandamanaji waliweka mahema kwenye Beinecke Plaza siku ya Ijumaa na kuandamana mwishoni mwa juma, wakitoa wito kwa chuo kikuu cha Yale kusitisha uwekezaji wowote katika kampuni za ulinzi zinazofanya biashara na Israel.
Nadine Cubeisy, mwanafunzi wa Yale na mmoja wa waandalizi wa maandamano hayo, alisema inasikitisha kwamba "chuo kikuu hiki ninachoenda, ninachochangia na ambacho marafiki zangu wanatoa pesa kinatumia pesa hizo kufadhili ghasia."
Maafisa wa shule walisema walizungumza na waandamanaji kwa saa kadhaa na kuwapa hadi mwisho wa wikendi kuondoka Beinecke Plaza. Walisema waliwaonya tena waandamanaji Jumatatu asubuhi na kuwaambia kwamba wanaweza kukamatwa na kuadhibiwa, ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi, kabla ya polisi kuingia.
Wiki iliyopita, Chuo Kikuu cha Kusini mwa California kilichukua hatua isiyo ya kawaida ya kufuta hotuba iliyopangwa ya kuaga chuo 2024, kwa aliyekuwa amewaunga mkono hadharani Wapalestina. Chuo kikuu hicho kilitaja wasiwasi wa kiusalama katika uamuzi ambao ulisifiwa na baadhi ya makundi yanayounga mkono Israel lakini ukakosolewa na watetezi wa uhuru wa kujieleza.
Huko New York, maafisa walikabiliana na umati katika chuo cha NYU muda mfupi baada ya kuingia usiku, kwani mamia ya waandamanaji kwa masaa mengi walikuwa wamekaidi maonyo ya chuo kikuu kwamba watachukuliwa hatua ikiwa wangekosa kuondoka kwenye uwanja ambao walikuwa wamekusanyika.
Video kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha polisi wakishusha hema za waandamanaji katika eneo hilo.
Huku waandamanaji wakizozana na polisi na kupiga kelele wakisema, "Hatutaacha na hatutapumua.