Majeshi ya Israeli yamemuua mwanahabari wa kujitegema anayefanya kazi na Shirika la Habari la Anadolu.
Siku ya Ijumaa, majeshi ya Israeli yalizingira kambi ya wakimbizi ya Al-Jadeed iliyoko katika eneo la Nuseirat na kutekeleza shambulio hilo.
Picha mjongeo zilimuonesha mtu mmoja aliyejeruhiwa vibaya akiwa amebebwa ndani ya machela, huku Abu Nabhan akijaribu kupiga picha tukio hilo kabla ya kushambuliwa na kupoteza maisha.
Shirika la Habari la Wafa lilithibitisha kifo cha Abu Nabhan.
Hadi kufikia sasa, jumla ya wanahabari 203 wameuwawa katika mashambulizi mfululizo ya Israeli dhidi ya Gaza toka Oktoba 7, 2023, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa kwa mashambulizi hayo.
TRT Afrika