Majeshi ya Israeli yanadai kumuua kiongozi wa kamandi ya Hamas, Mohammed Deif, katika shambulio la anga, mwezi Julai.
Israeli ilimlenga Deif katika shambulio la Julai 13, katika eneo la kusini Gaza katika mji wa Khan Younis, licha ya kutokuwepo kwa uthibitisho wa mauaji hayo.
Zaidi ya Wapalestina 90, wakiwemo wasio na makazi, waliuwawa katika shambulio, mamlaka za afya za Gaza zimesema.
Katika taarifa yake ya Alhamisi, jeshi la Israeli lilisema kuwa “kufuatia tathmini iliyofanyika, tunaweza kuthibitisha kuuwawa kwa Mohammed Deif katika shambulio hilo.”
TRT Afrika