Hospitali ya Uturuki nchini Lebanon yaanzisha kitengo cha majeruhi wa moto kutokana na mashambulizi ya Israeli

Hospitali ya Uturuki nchini Lebanon yaanzisha kitengo cha majeruhi wa moto kutokana na mashambulizi ya Israeli

Kulingana na Waziri wa Afya wa Lebanon, kitengo hicho kitasaidia kutibu majeruhi wa mashambulizi ya anga yanayofanywa na Israeli.
Uturuki imejitolea kujenga kitengo hicho kutokana mashambulizi ya anga yanayofanywa na Israeli./Picha: TIKA 

Waziri wa Afya wa Lebanon Firas Abiad amesema kuwa kitengo hicho kilichopo katika hospitali ya Kituruki mjini Sidon nchini Lebanon kitafunguliwa siku ya Jumanne ili kuweza kutoa matibabu kwa majeruhi wa moto kutokana na mashambulizi dhidi ya Lebanon yanayoendelea.

"Kitengo cha kutibu walioungua kitafunguliwa kesho," Abiad aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Beirut siku ya Jumatatu.

"Hospitali hii itakuwa ni ya rufaa kwa ajili ya majeruhi walioungua," aliongeza.

Waziri wa Lebanon aliishukuru Uturuki kwa msaada huo kupitia Taasisi ya Ushirikiano na Uratibu ya Uturuki (TIKA).

Hali mbaya ya afya Lebanon

Kulingana na Abiad, kitengo hicho kitakuwa na sehemu ya dharura na nyingine kwa ajili ya majeruhi, vyumba viwili vya upasuaji, vyumba vinne vya wagonjwa mahututi, vitanda vinne na kliniki maalumu kwa ajili ya majeruhi.

Uturuki ilijitolea kujenga hospitali kufuatia mashambulizi ya Israeli dhidi ya Lebanon mwaka 2006. Hospitali hiyo ilijengwa mwaka 2010.

Kulingana na Waziri wa Afya wa Lebaon, hospitali nane nchini humo zilisitisha huduma kutokana na mashambulizi ya Israeli dhidi ya sekta ya afya.

Israeli imezidisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya Lebanon toka mwishoni mwa mwezi Septemba dhidi ya kile inachokiita Hezbollah.

Watu wapatao 3,000 wameuwawa na wengine zaidi ya 13,000 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israeli yaliyoanza mwezi Oktoba 2023, kulingana na vyanzo vya afya nchini Lebanon.

Takriban watu 3,000 wameuawa na zaidi ya 13,300 kujeruhiwa katika ushindi wa Israel tangu Oktoba 2023, kulingana na mamlaka ya afya ya Lebanon.

Israeli iliongeza mzozo huo kwa uvamizi kusini mwa Lebanon mnamo Oktoba 1 mwaka huu.

TRT Afrika