Kikosi cha waokoaji wa Uturuki kimeanza utafutaji wa kina katika jela ya Syria ya Sednaya, msemaji wa kitengo cha majanga cha Uturuki AFAD ameiambia AFP.
Jela hiyo iliyopo kaskazini mwa Damascus, imekuwa ishara ya ukiukaji wa haki za binadamu katika utawala wa Assad, hasa tangu kuanza kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoibuka 2011.
Wafungwa waliokuwa katika jela hiyo, ambayo ilikuwa ni sehemu ya mauaji, mateso na kupotezwa, waliachiliwa wiki iliyopita baada ya utawala wa Assad kuanguka Disemba 8.
(AFAD) imesema Jumatatu kwamba imetuma kikosi cha takriban watu 80 kusaidia katika upekuzi "wa watu wanaodhamiwa kukwama katika jela ya Sednaya."
Jela hiyo inaaminika, huenda ikawa imeenda chini zaidi, na kujenga dhama kwamba kuna wafungwa zaidi ambao hawajaonekana.
Lakini, Taasisi ya Wanaoshikiliwa na Watu Waliopotea wa Jela ya Sednaya (ADMSP) wana maoni tofauti kuhusu fununu hizo.
AFAD imesema kikosi hicho, ambacho kimebobea katika utafutaji wa mijini na uokoaji, kitafanya kazi kwa kutumia "vifaa vya hali ya juu", limeripoti Shirika la anadolu.
Wafanyakazi wa kitengo cha dharura cha 'Syria White Helmets' kimefanya ukaguzi katika jela hiyo na kufunga shughuli hiyo Jumanne, kwa kusema wameshindwa kupata wafungwa zaidi.
Waokoaji wametoboa matundu katika kuta lakini hawakupata kitu, huku maelfu ya wanafamilia wakionyesha kukata tamaa-bila kujua iwapo ndugu zao wameuawa au hawataonekana tena.
ADMSP imesema waasi waliwaachia zaidi ya wafungwa 4,000 kutoka Sednaya, ambayo Amnesty International imeielezea kama "machinjo ya binadamu".
Shirika la Uokoaji lililopo kusini mwa Uturuki, linaamini zaidi ya wafungwa 30,000 wamefariki kwa kuuawa, mateso, njaa au kukosa matibabu kati ya 2011 na 2018.