Israel iko tayari kubadilisha mkakati wake wa mpaka na Lebanon, anasema Waziri Mkuu Netanyahu. / Picha: AA

Jumatatu, Juni 24, 2024

0120 GMT - Israel inajiandaa kubadili hali kwenye mpaka wake na Lebanon lakini inatumai hakutakuwa na haja ya kufanya hivyo, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema, akizungumzia makabiliano yanayoendelea ya jeshi na kundi la Hezbollah la Lebanon.

Akizungumza na Idhaa ya 14 ya Israel kuhusu uwezekano wa vita kamili na Hezbollah, Netanyahu alisema ikibidi, "tutakabiliana na changamoto hii pia. Tunaweza kupigana katika nyanja kadhaa. Tumejiandaa kwa hili.”

Kuhusiana na vita vya Gaza, alisema awamu ya mapigano makali inakaribia mwisho, lakini vita havitaisha hadi pale Hamas watakapoacha kudhibiti tena eneo hilo.

Netanyahu alisema kuwa Tel Aviv inataka kuanzisha "koo za ndani" kutawala Gaza.

Pia alisema kuwa kuanzisha upya makaazi ya Waisraeli huko Gaza "si jambo la kweli" na hakutatimiza malengo ya vita.

0200 GMT - Mlipuko wa bomu wa Israeli katika Jiji la Gaza waua wafanyikazi 2 wa wizara ya afya

Wapalestina wawili wanaofanya kazi katika Wizara ya Afya waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulio ya anga ya Israeli kwenye kliniki ya matibabu katikati mwa jiji la Gaza.

Shirika la ulinzi wa raia la Gaza lilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba "timu zake zilipata miili ya mashahidi wawili wanaofanya kazi katika Wizara ya Afya na watu wengi waliojeruhiwa kutokana na ndege za Israel zilizokuwa zikilenga Kliniki ya Al Daraj," bila kutoa maelezo zaidi.

0021 GMT - Waisraeli walijeruhiwa kwa kombora la kifaru lililorushwa kutoka kusini mwa Lebanon

Waisraeli wawili walijeruhiwa wakati nyumba moja ilipopigwa na kombora la kifaru lililorushwa kutoka Lebanon.

"Watu wawili walijeruhiwa kidogo" na kombora la kifaru lililorushwa kuelekea mji wa kaskazini mwa Israel wa Metula, Redio ya Jeshi la Israel ilisema kwenye X.

Helikopta iliripotiwa kuwahamisha majeruhi hadi katika Kituo cha Matibabu cha Rambam huko Haifa. Hakujawa na maoni ya mara moja kutoka kwa upande wa Lebanon juu ya ripoti hiyo.

TRT World