Na Mir Seeneen
Licha ya mabadiliko ya hivi majuzi kuelekea upatanisho, India na China zinaonekana kuwa wapinzani wakubwa kuliko hapo awali.
Mataifa hayo mawili yamekuwa na mizozo ya kidiplomasia katika miaka ya hivi karibuni, huku Rais wa China Xi Jinping akikataa kuhudhuria mkutano wa kilele wa G-20 wa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi 2023.
Kwa upande wake, Modi hakuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai huko Kazakhstan.
Hata hivyo, mataifa hayo mawili yalikubali makubaliano ya mpaka yaliyojadiliwa vikali kuhusu eneo linalozozaniwa la Ladakh mwezi Oktoba. Ikiashiria makubaliano hayo, Wizara ya Mambo ya Nje ya India (MEA) iliangazia uhusiano wake ulioboreshwa na Beijing mnamo Desemba.
Lakini majaribio kama haya ya amani hayana uwezekano wa kuzuia mzozo unaoongezeka unaoendelea katika ulimwengu wa mtandao kati ya mataifa hayo ya Asia yenye watu zaidi ya bilioni mbili.
Hatua hiyo ilionekana kama uchokozi katika vita vya mtandaoni vinavyoendelea, katikati ya mzozo wa mpaka wa India na Uchina huko Ladakh.
Kuendelea kwa mijadala katika mitandao ya kijamii nchini India kulichochea tu uwanja huu wa vita vya kidijitali, huku programu za Wachina zikilaumiwa kwa kuwa na "maudhui haramu" na matishio ya usalama wa taifa yanayoweza kutokea.
Kwa upande China, wafafanuzi wake walianzisha vita vyao vya uzalendo, wakichapisha makala katika machapisho yanayomilikiwa na serikali ambayo yalikashifu masimulizi ya India yenye uzalendo wa kupita mpaka.
Pia iliwaonya juu ya matokeo, ikiwa ni pamoja na kuchochea suala la Kashmir katika Umoja wa Mataifa na kuanzishwa kwa operesheni za kijeshi huko Ladakh na Arunachal Pradesh.
Vita hivi vya maneno vilisababisha New Delhi kuweka vikwazo zaidi kwa programu maarufu za Kichina kama vile TikTok katika jina la kampeni yake ya "Make in India", ikishajiisha India watengeze vitu vyao wenyewe, ambapo kwa mara ya kwanza, programu za Kihindi zilianza kutawala mtandao wa India.
Ushindani huo unapunguza maendeleo ya kitaifa yenye ustaarabu wa zamani ambao hapo awali ulinufaika kutokana na mabadilishano ya kibiashara na kitamaduni.
New Delhi inaona Beijing kama mshindani wake mkubwa, na kusababisha utawala wa India kusimamisha safari za moja kwa moja za ndege kwenda China, kusitisjha utoaji wa visa, kuwafukuza waandishi wa habari na kupunguza uwekezaji wa Wachina nchini India.
India pia imeweka vizuizi kwa mashirika ya kiraia, majadiliano ya vyombo vya habari, programu za kubadilishana wanafunzi, shughuli za kitamaduni na mikutano ya sanaa na ufundi, na kufanya iwe vigumu kwa watu wa kila siku wa India na China kuingiliana.
Kabla ya ushindani huu, nchi zote mbili zilifurahia uhusiano mzuri katika miaka ya 90. Waliunda soko lao lao wenyewe: China iliyo na (semiconductors) teknolojia katika wa vifaa vya elektroniki kama vile chipu za kompyuta, na India ikishughulukia programu (software).
Lakini ikisaidiwa na ujuzi wa ufundi, Beijing iliongeza maradufu mapato yake kwa kila mtu ikilinganishwa na wapinzani wake wa Asia. Hii ilichochea uhasama, licha ya nchi hizo mbili kutia saini mkataba wa amani wa 1993 na makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi wa mpaka wa 2013.
Masuala mengine
Vita vya mtandaoni vinaonekana kuwa dhihirisho la masuala mazito ambayo India na China zimetofautiana kwa miongo kadhaa, ikijumuisha mizozo ya maeneo.
Kwanza, kuna uwepo wa kijeshi wa Beijing kwenye mpaka wa Ladakh, na pia katika Bahari ya Hindi, ambapo New Delhi inaituhumu China kwa kuendesha meli za kijasusi.
Beijing haikusita kwani ilionyesha kutoridhika na uungwaji mkono wa India kwa "jimbo lililoasi" la Taiwan. China pia ilishutumu New Delhi kwa kuingilia suala la Tibet mnamo 2019 kwa kumhifadhi kiongozi wa Buddha, Dalai Lama, anayeonekana na Wachina kama mtu anaye endeleza kampeni za kujitenga.
Kupinganai kwa nchi hizi mbili pia kunafafanua ugomvi kati yao. Kama sehemu ya pande mbili zinazohasimiana, India inaunga mkono Indo-Pacific Quad, huku Uchina ikiweka uzito wake nyuma ya Mpango wa ‘‘Belt and Road’’.
Kama mwanachama wa BRICS - mrengo wa kimataifa unaojumuisha Brazili, Urusi, India, China na Afrika Kusini - China ilitambulishwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja kama nchi dhidi ya Magharibi"anti-West" na Modi wakati wa kikao cha faragha Oktoba hii.
Wasiwasi mkubwa wa Waziri Mkuu wa India ni kupungua kwa ushawishi wa New Delhi katika kongamano hilo, huku Beijing na Moscow zikifuatilia mipango yao ya upanuzi wa kimataifa.
Mapambano ya Kashmir
Lakini anayetamani kuwa "Vishwa Guru" - kiongozi wa ulimwengu - "India mpya" ya Modi inakataa kuchukua nafasi ya pili barani Asia. Nchi inapinga waziwazi Ukanda wa Kiuchumi wa China-Pakistani katika Kashmir inayosimamiwa na Pakistan na inaendelea uchokozi wa Beijing huko Arunachal Pradesh.
China kwa upande mwingine inapinga uamuzi wa upande mmoja wa New Delhi kubadilisha mienendo ya eneo la migogoro huko Kashmir.
Mnamo Agosti 2019, New Delhi ilibatilisha hadhi maalum kwa Kashmir iliyozozaniwa na kuitambua Ladakh kama eneo tofauti. China ilipinga hatua hiyo ikisema inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu Jammu na Kashmir.
Hasira hii iliibuka baadaye huko Ladakh, ambapo Jeshi la Ukombozi la Watu lilipigana na Jeshi la India katika kile kilichoitwa makabiliano mabaya zaidi tangu vita vya 1962 vya Sino-India.
Miaka mitano baadaye, huku mvutano wa mpakani ukianzisha mwelekeo mpya barani Asia, waziri wa mambo ya nje wa India alitaka kufuatwa kwa sheria zilizopitishwa za kupunguza kwa makabiliano kwenye mpaka.
Hata hivyo, wengi nchini India wanaona hii kama njia ya kimbinu ya kurudi nyuma wakati vita vya Ukraine vimeileta China karibu na mshirika wa zamani wa ulinzi wa India, Urusi.
Hatua ya Beijing inachochewa na ushirikiano wa Marekani na India kuhusu usafirishaji wa majini na teknolojia mbovu. Wakati mazungumzo ya amani na juhudi za kidiplomasia zikiendelea, ushindani kati ya India na China katika anga ya mtandao bado ni sehemu kubwa ya vita.
Vita vya kidijitali, vinavyochochewa na masuala ya usalama wa kitaifa na ushindani wa kiuchumi, huenda vikaongezeka, huku nchi zote mbili zikilenga kudhibiti anga ya mtandao na ushawishi wa kimataifa.
Kwa sasa, mabadiliko ya kimkakati katika mtazamo wa India kwa Uchina, ingawa sio makubwa, yanasisitiza ushindani unaokua kati ya mataifa hayo mawili - ushindani ambao hauonyeshi dalili ya kupungua hivi karibuni.
Mwandishi, Mir Seeneen ni mwandishi wa kutoka Kusini-Asia, makala yake imechapishwa katika The Guardian, Al Jazeera, The Diplomat Magazine na SAAG.@MirSeeneen
Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayawakilishi lazima maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.