Hospitali tatu pekee zimesalia kaskazini mwa Gaza, zikiwahudumia takriban watu 900,000 eneo hilo, nazo zinakaribia kuanguka, afisa wa juu ameonya.
"Ni hospitali tatu tu ndizo zinazofanya kazi katika ukanda wa kaskazini wa Gaza, ambazo ni Al Maamadani, Al Awda, na Kamal Adwan," Bursh alisema, akionya "kuanguka kwao."
"Viwango vya misaada ya matibabu na mafuta iliyofika Gaza, haswa maeneo ya kaskazini mwa ukanda huo, ni vidogo sana na havitoshi, kwa kuzingatia hali mbaya ya kiafya ya hospitali," Munir Al Bursh, mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Afya Gaza, aliiambia Anadolu siku ya Jumapili.
"Dawa na vifaa vya matibabu lazima viletwe Gaza kwa wingi, tukizingatia hali mbaya ya kiafya katika ukanda huo," aliongeza.
Aidha, alisisitiza kuwa " kuna haja ya kuimarisha mfumo wa afya huko Gaza na mikoa ya kaskazini na kutoa huduma za afya za kutosha."
Alifafanua kuwa hali ya afya ya Gaza kwa ujumla, kuwa "janga kubwa na kukosa mahitaji muhimu ya afya."
Alhamisi iliyopita, ofisi ya vyombo vya habari vya serikali huko Gaza ilisema kuwa hospitali 26 na vituo vya afya 55 katika eneo hilo havikuwa na uwezo wa kutoa huduma.
Vikosi vya Israel pia vililenga Ambulansi 55 ya kubebea wagonjwa, huku makumi mengine yakikosa huduma kutokana na uhaba wa mafuta.
Ubadilishanaji wa wafungwa huku kukiwa na mzozo
Kusitishwa kwa siku nne kufanikisha misaada ya kibinadamu iliyosimamiwa na Qatar kulianza Ijumaa, pamoja na kusimamishwa kwa muda mashambulio ya Israeli huko Gaza.
Usitishaji huo pia ulikusudiwa kurahisisha uwasilishaji wa misaada zaidi kwenye eneo lililozingirwa.
Ingawa Israeli ilikuwa imeondoa kizuizi chake kamili kilichowekwa mara tu baada ya Oktoba 7, iliruhusu tu misaada iliyohitajika sana kuingia, sehemu ndogo ya kile kilichotolewa kabla ya wakati huo.
Israel na Hamas zilibadilisha Waisraeli 41 na raia wa kigeni kwa Wapalestina 78 waliokuwa magereza ya Israel katika matukio mawili ya ubadilishanaji wafungwa uliofanywa katika siku mbili za kwanza za mapumziko ya siku nne za kibinadamu.
Israel ilianzisha kampeni kubwa ya kijeshi huko Gaza kufuatia shambulio la kuvuka mpaka la Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba.
Tangu wakati huo, Israel imeua Wapalestina 14,854, wakiwemo watoto 6,150 na zaidi ya wanawake 4,000, kulingana na wizara ya afya katika eneo hilo.
Idadi rasmi ya vifo vya Israeli mpaka sasa ni 1,200.