Jumla ya wahudumu 11 wa afya wameuawa katika mashambulizi ya Israel. Picha: AA

Na Takunda Mandura

Msimamo wa nchi za Magharibi juu ya mashambulizi yanayoendelea ya Gaza na Israel ni ishara tosha ya ''halisi'' ya msimamo wa kibaguzi, Balozi wa Palestina nchini Zimbabwe, Tamer Almassri alisema.

Balozi Almassri alielezea vitendo vya Israel kama ''mauaji ya halaiki'' na akashutumu kutochukua hatua kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu juu yake. Kumekuwa na wito kwa mahakama ya ICC kuchukua hatua dhidi ya mashambulizi ya Israel dhidi ya raia huko Gaza.

"Kwa bahati mbaya, ICC haichukui hatua zozote dhidi ya wahalifu wa Israel kwa sababu wao si Waafrika," aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare.

“Kama walikuwa Waafrika, wangewakamata na kuwaita mahakamani, lakini kwa sababu hawako na ngozi nyeusi, wana uhuru wa kufanya mauaji ya kimbari wanayotaka,” aliongeza.

Idadi ya vifo huko Gaza inaendelea kuongezeka. Takriban Wapalestina 4,100 wameuawa - wengi wao wakiwa wanawake na watoto - tangu Israel ilipoanzisha kampeni yake ya kulipua mabomu takriban wiki mbili zilizopita, Wizara ya Afya ya Palestina ilisema.

Hakuna mahali salama

"Hakuna mahali, hakuna sentimita iliyo salama katika Ukanda wa Gaza" alisisitiza mwanadiplomasia huyo.

Eneo lililozuiwa lenye ukubwa wa kilomita za mraba 365 lina wakazi milioni 2.2.

Kulingana na Balozi Almassri, Israel haizingatii sheria za kimataifa na haki za binadamu.

"Tungependa kusisitiza kuwa taifa la Israel ni taifa lililoanzishwa kwanza kabisa kupitia vurugu na bado linatumia vurugu hizi kwa njia za kutisha dhidi ya watu wetu," aliongeza.

Pia alizishutumu nchi za Magharibi kwa ''na msimamo wa kibaguzi'' akisema zimefumbia macho''mashambulio ya Israel dhidi ya Wapalestina ambayo ni tofauti na majibu yao kwa vita vya Urusi na Ukraine.

TRT Afrika