Wanaharakati na wanafunzi wakiwa kwenye kambi ya maandamano katika Chuo Kikuu cha George Washington huko Washington DC, Mei 1, 2024. /Picha: Reuters

Na

Moataz Salim

Wanafunzi kote Marekani wanaporejea katika vyuo vikuu muhula huu, wengi wanakabiliwa na vikwazo upya katika suala la haki yao ya kuandamana, kupinga kwa amani na kueleza kutoridhika kwao na uungaji mkono wa vyuo vikuu kwa Israeli.

Katikati ya Washington, DC, chuo kikuu changu kimekuwa kikishughulika na kusaliti kanuni za msingi za uhuru wa kujieleza ambazo daima kimedai kushikilia.

Chini ya uongozi wa Rais Ellen Granberg, Chuo Kikuu cha George Washington (GWU) kimeshiriki katika kampeni iliyolengwa dhidi ya wanafunzi wake wa Kipalestina, Waarabu na Waislamu.

Chuo kikuu hiki, ambacho kinadai kuwa kinara wa uhuru wa kujieleza, badala yake kimekuwa taasisi inayowasuta wale wanaothubutu kupinga mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza.

Hatua za GWU hadi sasa zimejumuisha kukamatwa kwa watu wengi; kusimamishwa kwa vikundi katika chuo kikuu, kama vile kikundi cha "Students for Justice in Palestine (SJP)" na "Jewish Voice for Peace (JVP)"; na hatua za kinidhamu zinazoendelea dhidi ya wanafunzi nikiwemo mimi mwenyewe.

Chuo cha GWU kinasaidia Israeli

Kupitia hatua hizi, chuo kikuu changu kimeonyesha msimamo wake juu ya mauaji ya kila siku, njaa na udhalilishaji wa Wapalestina na utawala wa Kizayuni wa Israeli. Kukataa kwa GWU kujiondoa kutoka kwa makampuni yaliyoshiriki katika kufadhili na kusaidia kwa silaha mauaji haya ya kimbari kunasisitiza zaidi uungwaji mkono wake.

Katika miezi ya hivi majuzi, sifa ya chuo kikuu ya kukuza mazingira ambayo sio tu ya uadui lakini ya ubaguzi wa kijamii dhidi ya jamii yangu imepata sifa mbaya.

Mapema mwezi huu, Baraza la Mahusiano ya Kiislam na Marekani (CAIR) liliteua GWU kama taasisi inayoongoza kwa unyanyasaji wake unaolenga "Wapalestina, Waislamu, Waarabu, Wayahudi, na wanafunzi wengine, wahadhiri, na wafanyikazi" ambao wamekuwa wakipinga mauaji ya halaiki ya Wapalestina huko Gaza.

Katika ripoti hii, Baraza la CAIR lilieleza kwa kina ukiukaji mkubwa wa uhuru wa kujieleza na kuongezeka kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya Wapalestina na chuki dhidi ya Uislamu katika zaidi ya vyuo 30 vya Marekani, huku GWU ikiorodheshwa kati ya tatu bora kwa "matukio mabaya zaidi ya vurugu" pamoja na Emory na UCLA.

Hali katika GWU ilikuwa mbaya sana hivi kwamba Mkurugenzi wa Utafiti na Utetezi wa CAIR, Corey Saylor, aliwataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho kuzingatia taasisi nyingine ambapo uhuru wa kujieleza na kitaaluma unaheshimiwa kikweli, badala ya kuwa ahadi tupu.

Ubaguzi wa muda mrefu

Haya si tukio jipya. Hata kabla ya kambi za Gaza, GWU ilikuwa na historia mbaya ya kuwalenga Wapalestina. Mnamo Mei 11 mwaka jana, Idara ya Elimu ya Marekani ilifungua uchunguzi rasmi kuhusu malalamiko ya kutumia kipengele cha "Title VI" inayodai kuwa GWU iliwabagua wanafunzi wa Kipalestina.

Na mnamo Novemba 2021, Palestina Legal, kikundi cha utetezi kilicholenga kutetea watu wanaounga mkono haki za Palestina, kilianzisha malalamiko ya haki za kiraia dhidi ya GWU kwa sababu chuo kikuu kusitissha nafasi ya uponyaji ya wanafunzi wa Palestina iliyoandaliwa na Ofisi yake ya ''Office of Advocacy and Support after Hillel'', baada ya shirika la chuo kikuu linalounga mkono Israeli, kuwasilisha malalamiko.

Usitshwaju huu ulimnyima mwanafunzi Mpalestina, aliyejeruhiwa alipokuwa akisoma kupitia mtandano katika Ukingo wa Magharibi, kupata huduma ya afya ya akili inayohitajika sana baada ya kupata kiwewe kikubwa.

Ndani ya saa 24 za kutangaza nafasi hiyo ya uponyaji, maafisa wa ngazi ya juu wa GWU waliingilia kati kuifunga, na kufichua sura ya kweli ya kutojali kwa chuo hicho kwa ustawi wa wanafunzi wake wa Kipalestina.

Katika mfano mwingine, mwaka jana, Dk. Lara Sheehi, profesa wa zamani wa saikolojia wa GWU, alilengwa wakati wa semina ya mtandaoni na wanafunzi wanaoiunga mkono Israeli kwa ajili ya kutetea haki za Wapalestina.

Nilikuwa katika darasa ambalo Sheehi alikuwa akifundisha wakati wanafunzi kadhaa walipotoa matamshi ya chuki dhidi ya Palestina, kama vile kuwataja raia wote wa Palestina waliouawa na jeshi la Israeli kuwa magaidi. Hakuna madhara yoyote dhidi ya wahusika yalitangazwa.

Hali hii ya chuki na kutovumiliana ambayo GWU imeruhusu kushamiri haina ubishi.

Kambi ya Gaza

Mnamo Aprili, wanafunzi waliweka kambi huko Gaza, wakitaka chuo kikuu kifute mashtaka ya awali dhidi ya waandaji wa wanafunzi wanaounga mkono Palestina; kulinda utoaji wahotuba ya Palestina kwenye chuo; kuachana na makampuni yanayouza teknolojia na silaha kwa utawala wa Kizayuni; kufichua mara moja uwekezaji wote unaofanywa kwa Israeli; na kukomesha ushirikiano wote wa kitaaluma na Israeli.

Badala ya kujibu madai haya, Rais Granberg na utawala wa chuo kikuu walichagua kuwaachilia maafisa wa polisi wa DC, kwa usaidizi wa Meya wa DC Muriel Bowser, kuvamia kambi hiyo kwa jeuri.

Ukatili wa polisi uliotokea ulikuwa wa kutisha, na wanafunzi wa Kipalestina na Waislamu walilengwa hasa. Mimi binafsi nilipigwa ngumi na polisi na kumwagiwa dawa ya pilipili huku nikijaribu kuwatawanya waandamanaji.

Wanafunzi wengine na wanajamii pia walitendewa unyama na polisi na kunyunyiziwa pilipili. Wakati wa uvamizi huu, GWU ilituma ujumbe wazi: ingependelea kutumia vurugu dhidi ya wanafunzi wake kuliko kujitenga na makampuni yanayohusika na mauaji ya halaiki.

Zaidi ya hayo, GWU awali iliwazuia wataalamu wa afya wa jamii na waangalizi wa kisheria kuingia kambini, na kuhatarisha zaidi usalama na haki za waliohudhuria.

Baada ya uvamizi huo mkali wa kambi, GWU ilionekana kuharibu mikeka ya maombi ya wanafunzi na chapa za Kurani zilzotafsiriwa, ikisisitiza kudharau kwake kabisa utu na uhuru wa kidini wa wanafunzi wake.

Watu 33 walikamatwa wakati wa msako huu wa kikatili, wakiwemo angalau wanafunzi wanane wa GWU, wanafunzi kadhaa kutoka vyuo vikuu vingine katika eneo la DC-Maryland-Virginia, na wanajamii wengine.

Wengi wanakabiliwa na adhabu kali ya kisheria kwa agizo la chuo kikuu—"amri ya kufukuzwa" chuo kwa muda wa miezi sita, inayowazuia kufikia kumbi za kulia chakula, maktaba na hata usafiri wa metro.

Mbali na mashtaka hayo ya kisheria, wanafunzi wanakabiliwa na hatua za kinidhamu kutoka chuo kikuu, na kuonyesha zaidi mtazamo wa kikatili na wa kuadhibu wa GWU kwa wale wanaopinga kushiriki kwake katika mauaji ya kimbari.

Kufuatia kukamatwa kwa watu hao, Mara Verheyden-Hilliard, mkurugenzi mtendaji wa ''Partnership for Civil Justice Fund'', ambaye shirika lake linawakilisha angalau mwanafunzi mmoja aliyekamatwa, alibainisha kwa usahihi katika taarifa yake: "Mashtaka haya ni nje ya utaratibu wa kawaida kuhusu kukamatwa kwa waandamanaji"zina msukumo wa kisiasa na zina nia ya kunyamazisha na kulipiza kisasi dhidi ya wanafunzi kwa sababu walitetea dhidi ya mauaji ya kimbari huko Gaza."

Mark Goldstone, wakili wa utetezi anayewakilisha wanafunzi kadhaa, alilaani amri hiyo wakati akizungumza na Washington Post na kuitaja kama ya "kupindukia, pana, na isiyokuwa ya lazima."

Ukandamizaji unaendelea Kwa kuhofia kuzuka upya kwa maandamano ya kuunga mkono Palestina katika muhula mpya, GWU mnamo Agosti 21, 2024, ilisitisha vikundi vya chuo kikuu vya ''Students for Justice in Palestine (SJP)'' na ''Jewish Voice for Peace (JVP)''.

Ukandamizaji huu wa wazi wa upinzani bado ni mfano mwingine wa nia ya chuo kikuu kuwanyamazisha wale wanaozungumza dhidi ya ushiriki wake katika mauaji ya kimbari.

Nakumbuka nikihisi kuwa mpweke na kuhuzunishwa na ukosefu wa chuo kikuu kukiri mauaji ya halaiki ya watu wangu, na vile vile kwa ukimya wa washiriki wengi wa wahadjiri na wanafunzi katika darasa langu.

Nimepoteza jamaa 161 kwenye mauaji ya kimbari huko Gaza. Kwa uanaharakati wangu kwa Gaza na Palestina, nilitendewa unyama na polisi kwa amri ya GWU.

Ninapoandika haya, naendelea na taratibu za kinidhamu licha ya kuwa nimepata likizo hadi Januari. Juhudi za chuo hicho kuzima sauti za wanafunzi wa Kipalestina hazitafaulu. Licha ya hatua zao za kuadhibu, wanafunzi na wanajamii waliandamana kupitia chuo cha GWU mwezi huu ili kudhihirisha kuwa mapambano ya haki na kujitenga na mauaji ya kimbari hayatanyamazishwa.

Ushauri kwa siku zijazo

Hakuna anayejua kitakachofuata, lakini jambo moja ni la uhakika: wanafunzi wa GWU, na pengine wale ambao bado hawajalengwa na hatua za kuadhibu, wataendelea kushinikiza chuo kikuu kuacha uungaji mkono wa mauaji ya halaiki na ukoloni wa walowezi.

Mamia ya wanajamii walihudhuria mkutano wa hivi punde, kuashiria kuwa watu wa DC na eneo la DMV wanaunga mkono wanafunzi wanaopinga mauaji ya kimbari.

Licha ya matumaini yangu katika vita hivi, ninawaacha na onyo: Kwa wanafunzi wa Kipalestina, Waarabu, na Waislamu wanaozingatia GWU kama chaguo la kupata elimu, ushauri wangu ni rahisi: usijiunge. GWU ni mahali pa hatari kwa wale wanaothubutu kupigana dhidi ya dhuluma.

Unafiki wa chuo kikuu, kuacha kwake kanuni za uhuru wa kujieleza, na kushiriki kwake katika mauaji ya halaiki huifanya kuwa mazingira ya hatari kwa mwanafunzi yeyote anayethamini haki za binadamu.

Mwandishi, Moataz Salim ni mwanafunzi wa Kipalestina aliyehitimu katika chuo cha DC kutoka Gaza akitetea kukomesha mauaji ya kimbari na ukombozi wa Palestina. Amejiunga na CODEPINK kila siku kwa muda wa miezi 3 ili kuwa sauti kwa watu wake. Pia amehusika katika uanaharakati katika chuo kikuu na ndani ya jumuiya ya eneo hilo, aliyejitolea kwa muda wa miezi 10 iliyopita kupigania ukombozi wa Wapalestina.

Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayawakilishi lazima maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT Afrika