Gabriel Boric atoa wito wa kushtakiwa Israeli kwa kuhusika na mauaji ya kimbari huko Gaza. /Picha: AFP

Rais wa Chile Gabriel Boric alisema siku ya Jumamosi, nchi yake inaungana na Afrika Kusini katika kesi iiiyowasilisha mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki inayoishutumu Israeli kwa "mauaji ya kimbari" katika vita vya Gaza.

Akizungumza na Bunge la Kitaifa, Boric alishutumu "hali mbaya ya kibinadamu" huko Gaza na kutoa wito wa "majibu madhubuti kutoka kwa jumuiya ya kimataifa."

"Chile itakuwa mshiriki na kuunga mkono kesi ambayo Afrika Kusini iliwasilisha dhidi ya Israeli mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko mjini Hague," Boric alisema.

ICJ inazingatia kesi ya Afrika Kusini, hapo awai iliamuru Israeli kufanya kila iwezalo kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki katika uvamizi wake huko Gaza.

Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa mwezi uliopita, iliiamuru Israeli kusitisha operesheni za kijeshi katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ambako Wapalestina waliokimbia makazi yao wanatafuta usalama kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Israeli.

'Vita haramu'

Kabla ya mashambulizi ya Rafah kuanza, Umoja wa Mataifa ulisema hadi watu milioni 1.4 walikuwa wamekita kambi kutafuta hifadhi katika jiji hilo.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), tangu wakati huo, watu milioni moja wamekimbia eneo hilo.

Chile imeitambua Palestina kama taifa huru tangu mwaka 2011, na Boric alishawahi kusema kuwa vita vya Gaza "havina uhalali" na "havikubaliki."

Israeli ilianzisha vita vyake vya anga na ardhini dhidi ya Gaza baada ya wapiganaji wa Hamas Israeli, na kuua watu 1,200 na kuwakamata zaidi ya mateka 250, kulingana na takwimu zilizotolewa na Israeli.

Shambulio la Israeli limeua takriban watu 36,379 huko Gaza, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, kulingana na wizara ya afya ya Palestina katika eneo hilo.

TRT World