Bolivia imejiunga na kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki inayodai mashambulizi ya Israeli Gaza yanakiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ya Umoja wa Mataifa, mahakama hiyo ilisema Jumatano.
Nchi hiyo ya Amerika Kusini ndiyo ya hivi punde kati ya mataifa kadhaa, zikiwemo Colombia, Libya, Uturuki, Uhispania na Mexico, zilizojiunga kuongeza uzito wao katika kesi dhidi ya Israeli, ambayo inakanusha vikali shutuma hizo.
Bolivia tayari ilitangaza mnamo Novemba kuwa inakata uhusiano wa kidiplomasia kwa kile ilichoelezea kama shambulio "isiyo sawa" la israeli dhidi ya Gaza. Wakati huo, Israeli ilishutumu hatua hiyo na kusema "kujisalimisha kwa ugaidi".
Zuia mauaji ya halaiki
Katika uamuzi wa Januari 26 ambao uligonga vichwa vya habari duniani kote, ICJ iliiambia Israeli kufanya kila iwezalo kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki wakati wa operesheni zake za kijeshi huko Gaza.
Mahakama pia imeiamuru Israeli kuhakikisha na bila kizuizi chochote kwa wachunguzi walioagizwa na Umoja wa Mataifa kuruhusiwa kuchunguza madai ya mauaji ya halaiki.
Afrika Kusini imerejea mara kadhaa kwa ICJ, ikisema kuwa hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo inalazimisha mahakama kutoa hatua zaidi mpya za dharura.
Katika uwasilishaji wake kwa mahakama uliowekwa wazi siku ya Jumatano, Bolivia ilisema: "Vita vya mauaji ya halaiki ya Israeli vinaendelea, na maagizo ya Mahakama yanasalia kuwa barua zisizokuwa na maana kwa Israeli."
Mamlaka ya ICJ Ingawa maamuzi ya ICJ ni ya lazima kisheria, mahakama haina njia madhubuti ya kuyatekeleza.
Katika uamuzi tofauti mwezi Julai, ICJ ilitoa "maoni ya ushauri" kwamba ukaliaji wa mabavu wa Israeli katika ardhi ya Palestina ulikuwa "haramu" na unapaswa kukomeshwa haraka iwezekanavyo.
Oparesheni ya kijeshi ya Israeli dhidi ya Gaza imeua takriban watu 42,010, wengi wao wakiwa raia, kulingana na takwimu zilizotolewa na wizara ya afya ya eneo linalosimamiwa na Hamas.
Umoja wa Mataifa umetaja takwimu hizo kuwa za kuaminika.
Shambulio la Oktoba 7
Mashambulizi hayo yalichochewa na shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,205 nchini Israeli, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya AFP iliyonakili takwimu rasmi za Israeli ambazo ni pamoja na mateka waliouawa wakati wakiwa mateka.
Israeli imezidisha mashambulizi kwenye ngome za Hezbollah nchini Lebanon tangu Septemba 23, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,150, kulingana na takwimu rasmi za AFP.