Erdogan alitoa pole kwa familia za marehemu na kuwatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa. / Picha: AA

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema uturuki iko tayari kusaidia Morocco iliyokumbwa na tetemeko la ardhi "kwa kila njia" inayowezekana.

"Kama nchi ambayo ilikumbwa na 'janga la karne' miezi sita iliyopita, tuko tayari kuwasaidia ndugu zetu wa Morocco kwa uwezo wetu wote," Erdogan aliambia mkutano wa wanahabari Jumapili baada ya mkutano wa kilele wa G-20 mjini New Delhi, India.

Takriban watu 2,012 waliuawa na 2,059 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo ya Afrika Kaskazini mwishoni mwa Ijumaa.

Watu walifariki kutokana na tetemeko hilo la ukubwa wa 7 katika kipimo cha Richter iliyotokea katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na El-Houz, Taroudant, Chichaoua, Tiznit, Marrakech, Azilal, Agadir, Casablanca na Youssoufia.

Erdogan alitoa salamu za rambirambi kwa waliopoteza maisha na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Taasisi na mashirika ya Uturuki yametayarisha timu ya kutoa misaada na uokoaji inayojumuisha watu 265 watakaotumwa Morocco kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi.

Mikoa kumi na moja kusini mwa Uturuki ilikumbwa na matetemeko mawili mnamo Feb.

TRT World