Uturuki "imewakata makali" jumla ya magaidi saba wa toka vikundi vya PKK/YPG, katika eneo la kaskazini mwa Iraq na Syria, Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema.
"Mashujaa wetu kutoka majeshi ya ulinzi yamewakata makali magaidi 3 wa PKK/YPG waliogundulika katika operesheni ya ngao ya Euphrates na Peace Spring kaskazini mwa Syria na magaidi wengine wa kikundi cha PKK, waliobainika katika operesheni ya Claw-Lock zone," ilisema Wizara hiyo kupitia ukurasa wake wa X siku ya Jumapili..
Mnamo mwaka 2022, Uturuki ilizindua Operesheni Claw-Lock yenye kulenga maficho ya kikundi cha kigaidi cha PKK katika maeneo ya kaskazini mwa Iraq ya Metina, Zap, na Avasin-Basyan.
Operesheni zenye mafanikio
Kikundi cha kigaidi cha PKK kinajulikana kwa kutumia eneo la kaskazini mwa Iraq karibu na mpaka wa Uturuki, kama sehemu ya kujificha na kupanga mashambulizi dhidi ya Uturuki na kaskazini mwa Syria.
Tangu 2016, Ankara imeendesha operesheni tatu zenye mafanikio za kupambana na ugaidi katika mpaka wake kaskazini mwa Syria ili kuzuia uundaji wa ukanda wa ugaidi na kuimarisha amani ya wenyeji wa maeneo hayo : Ngao ya Euphrates (2016), Tawi la Olive (2018), na Spring ya Amani (2019).
Katika kampeni yake ya kigaidi ya miaka 40 dhidi ya Uturuki, kikundi cha PKK kimeorodheshwa kama kikundi cha kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, kikiwa kimehusika na vifo vya watu zaidi ya 40,000, wengi wao wakiwa ni akinamama na watoto. YPG ni tawi la PKK lililoko Syria.