Kalin alitoa salamu za rambirambi kwa Haniyeh baada ya dada yake kuuawa katika shambulizi la Israel na kwa watu wa Palestina waliouawa katika mashambulizi yanayoendelea. / Picha: Jalada la AA

Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) na mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas ya kikundi cha Palestina wamejadili maendeleo ya hivi karibuni katika mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza.

Ibrahim Kalin wa MIT na Ismail Haniyeh wa Hamas pia walijadili hatua za kupata usitishaji mapigano wa kudumu, ubadilishanaji wa wafungwa-wafungwa, na uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu katika mkoa huo, kulingana na habari iliyopatikana kutoka kwa maafisa Jumapili.

Kalin alitoa salamu za rambirambi kwa Haniyeh baada ya dada yake kuuawa katika shambulizi la Israel na kwa watu wa Palestina waliouawa katika mashambulizi yanayoendelea.

Aidha alisema Uturuki itaendelea kusimama pamoja na Wapalestina.

Ikipuuza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano, Israel imekabiliwa na shutuma za kimataifa kutokana na kuendelea na mashambulizi ya kikatili dhidi ya Gaza tangu shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la muqawama la Palestina, Hamas.

Zaidi ya Wapalestina 37,800 wameuawa huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 86,800 wamejeruhiwa, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.

Zaidi ya miezi minane ya vita vya Israel, maeneo makubwa ya Gaza yapo kwenye magofu huku kukiwa na kizuizi cha chakula, maji safi na dawa.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo uamuzi wake wa hivi punde uliiamuru Tel Aviv kusitisha mara moja operesheni yake huko Rafah, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni 1 walitafuta hifadhi kutokana na vita kabla ya kuvamiwa Mei 6.

TRT World