Uturuki yatuma salamu za rambirambi, yatoa msaada kufuatia mafuriko makubwa nchini Kyrgyzstan

Uturuki yatuma salamu za rambirambi, yatoa msaada kufuatia mafuriko makubwa nchini Kyrgyzstan

Uturuki imethibitisha utayari wake wa kutoa msaada kwa nchi ya  Kyrgyzstan kufuatia janga la mafuriko.
Mafuriko makubwa yamekumba mji wa Nukat katika jimbo la Osh nchini humo/ Picha: AA  

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imeonesha masikitiko yake kufuatia mafuriko makubwa yalioukumba mji wa Nukat katika jimbo la Osh ndani ya Jamhuri ya Kyrgyz, tukio lililosababisha upotevu wa maisha ya watu wengi.

"Tumesikitishwa sana na vifo vya watu na mchakato wa kuwaokoa wengine wengi unaendelea," ilisema Wizara hiyo kupitia ukurasa wake wa X siku ya Jumapili.

Taarifa hiyo iliongeza, "Tunawaombea rehema ya Mungu wale wote waliopoteza maisha na tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa watu wa Kyrgyzstan."

Uturuki imethibitisha utayari wake wa kutoa msaada kwa nchi ya Kyrgyzstan kufuatia janga hilo la mafuriko.

TRT Afrika