Yilmaz Behraresh alitumia jina la siri la Osman Nuri Ocakli alipokuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la MLKP  / Photo: AA

Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) limemkata makali Yilmaz Behraresh, anayejulikana pia kama Osman Nuri Ocakli, katika eneo la Ayn Al Arab nchini Syria, vyanzo vya usalama vilisema Jumamosi.

Ujasusi wa Uturuki umefuatilia mienendo ya Ocakli kwa muda mrefu na kubainisha eneo lake kupitia mawakala ambao hawakutambulishwa.

Ocakli alikuwa mmoja wa wafuasi wa chama cha Kikomunisti cha Marxist-Leninist (MLKP) Syria na alikuwa akitafutwa katika Kundi Nyekundu.

Ocakli alihusika kwenye mashambulizi mengi nchini Uturuki, ikiwa ni pamoja na shambulio la 2022 kwenye gari lililokuwa na walinzi wa magereza katika mkoa wa Kaskazini-Magharibi wa Bursa.

'Alikuwa katika kundi nyekundu kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa na Uturuki,' vyanzo vilisema.

Pigo kubwa kwa MLKP

Kifo cha Ocakli kinaonekana kuwa pigo kwa kundi hilo la kigaidi, na kufanya iwe vigumu kwao kutekeleza mashambulizi.

Mnamo Januari 2023, ujasusi wa Uturuki ulimkata makali mtendaji mkuu wa MLKP nchini Syria, Ahmet Shoresh, ambaye pia alijulikana kama Zeki Gurbuz.

Alifanya kazi kama kiongozi wa FESK, mrengo wa kijeshi cha MLKP, tangu 2000.

Akiwa na uhusiano wa karibu na shirika la PKK, Ocakli alihamia eneo la Qandil la Iraq mnamo Novemba 2014 na kuanza kutekeleza shughuli za kigaidi katika eneo la Rasulayn nchini Syria mnamo 2015.

Kufikia Aprili 2018, gaidi aliyehusika na uvukaji kwa njia isiyo halali kati ya Uturuki na Syria chini ya MLKP, alikua mtu wa karibu wa Bayram Namaz, aliyeitwa Baran, aliyesemekana ni kiongozi wa zamani wa MLKP Syria.

Akawa “mtu wa 3 wa shirika hilo Syria.”

Baada ya Bayram Namaz kukatwa makali mwaka wa 2019, Ocakli alianza shughuli zake kama msaidizi wa Zeki Gurbuz, maarufu kama " Ahmet Sores", ambaye aliteuliwa kama afisa wa Syria wa MLKP, na kuendelea na shughuli zake huko Ayn ​​al-Arab mwaka jana.

MLKP ilianzishwa mnamo 1994 na iliongezwa kwenye orodha ya magaidi na Uturuki mnamo 2007.

Kundi hilo la kigaidi linahusika na mashambulizi mengi Uturuki na Kaskazini mwa Syria, ikiwa ni pamoja na shambulio la bomu la mwaka 2004 la basi mjini Istanbul iliyowauwa raia watatu.

TRT Afrika na mashirika ya habari