Nuh Yilmaz amesisitiza umuhimu wa kuongeza shinikizo kwa Israeli na washirika wake kwa ajili ya haki ya Palestina na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono Palestina./ Picha: AA 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Nuh Yilmaz ameilaani vikali serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa vurugu za kikanda, na kuiita ya kibaguzi.

Wakati wa mkutano wa Umoja wa nchi za Kiislamu (OIC) uliofanyika Jeddah siku ya Jumatano, Yilmaz aliituhumu utawala wa Netanyahu kwa kuwa wa kibaguzi na wenye itikadi kali, akidai kuwa imeitumbukiza kanda hiyo katika vurugu kubwa.

Aligusia mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh kama mfano halisi, akisema kuwa mauaji hayo yametia dosari juhudi za upatikanaji wa amani.

Yilmaz alituma salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Haniyeh, aliyeuwawa nchini Iran, Julai 31 na kukiita kitendo hicho kama cha aibu kilichokiuka utawala wa Iran.

Alisema kuwa hatua za Israeli zinatishia eneo hilo na mfumo dhaifu wa kimataifa. Yilmaz pia alisisitiza uungaji mkono wa Uturuki kwa kikundi cha Palestina na kusisitiza kwamba kadhia ya Palestina bado ni imara, licha ya kuendelea uchokozi wa Israeli.

Suluhisho la dola mbili

Akiangazia uvamizi unaoendelea wa Israeli katika maeneo ya Wapalestina, Yilmaz alisisitiza kwamba amani ya kweli katika Mashariki ya Kati inaweza kupatikana tu kwa kukomesha uvamizi huu na kutekeleza suluhisho la mataifa mawili kwa msingi wa mipaka ya 1967.

Pia amekosoa hatua ya Israeli ya kukataa wito wa kimataifa wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza na kuzuia misaada ya kibinadamu, akibainisha kuwa bunge la Israeli hivi karibuni limepitisha sheria zinazokataa kuanzishwa kwa taifa la Palestina na kuliteua shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kuwa shirika la kigaidi.

Yilmaz alionya kuwa ikiwa Israel ihaitazuiliwa, Netanyahu anaweza kuongeza wigo wa mzozo huo, na kusababisha madhara makubwa kwa eneo hilo na kwingineko.

Vile vile aliikosoa jumuiya ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuzuia umwagaji damu na kulaani wajumbe wa Bunge la Marekani kwa kumpigia makofi Netanyahu katika ziara yake ya hivi majuzi mjini Washington akihoji iwapo wanashangilia mauaji ya halaiki.

TRT Afrika