Ziara ya siku mbili ya Abbas mjini Türkiye, kuanzia Jumatano, inajumuisha mkutano na Erdogan katika siku ya kwanza, ikifuatiwa na hotuba ya bunge siku iliyofuata. / Picha: AA

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amewasili Ankara na amekutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Marais hao walikutana Ikulu siku ya Jumatano katika mji mkuu wa Uturuki, ambapo mkutano huo ulifungwa kwa vyombo vya habari.

Abbas atahutubia bunge la Uturuki siku ya Alhamisi katika kikao cha dharura kilichoandaliwa kuonesha msaada kwa ajili ya Palestina.

Abbas ataongelea mashambulizi ya Israel kwenye maeneo ya Palestina, hususan Gaza, wakati wa hotuba yake. Hotuba hiyo itatafsiriwa kwa Kiingereza, Kituruki, na Kifaransa kwa wakati mmoja.

Rais Erdogan atahudhuria kikao hicho, kuonesha mshikano wake na Palestina.

Ziara ya siku mbili ya Abbas nchini Uturuki, inayoanza Jumatano, inajumuisha mkutano na Erdogan siku ya kwanza, ikifuatiwa na hotuba bungeni siku inayofuata.

Licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano, Israel imekabiliwa na ukosoaji wa kimataifa katikati ya mashambulizi yake makali ya kudumu Gaza tangu shambulio la Oktoba 7 mwaka jana na kikundi cha upinzani cha Palestina, Hamas.

Takriban Wapalestina 40,000 wameuawa na Israel huko Gaza tangu wakati huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 92,000 kujeruhiwa, kulingana na mamlaka za afya za Gaza.

Zaidi ya miezi kumi yamepita tangu kuanza kwa vita vya Israel, maeneo makubwa ya Gaza yamebaki magofu wakati kumekuwepo na vizuizi vya chakula, maji safi, na dawa.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambapo uamuzi wake wa hivi karibuni uliitaka isitishe mara moja mashambulizi yake katika mji wa kusini wa Rafah, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni moja walikuwa wametafuta hifadhi kutokana na vita kabla ya kuvamiwa tarehe 6 Mei.

TRT World