Mabango yenye ujumbe tofauti katika lugha za Kituruki, Kiarabu na Kiingereza  zilizosomeka  "Kuna mauaji ya Kimbari Gaza" "Israeli isitishe mauaji ya kimbari ," na "Mauaji yasitishwe watoto wasiendelee kufa." / Picha: AA  

Jiji la Istanbul limeshuhudia umati wa watu wakikusanyika katika kwenye bustani ya Ayasofya kwa ajili ya "Wosia wa Mwisho kutoka kwa shahidi uliondaliwa na Jukwaa la Wapalestina.

Mamia kwa maelfu waliandamana mjini Istanbul Jumamosi, Agosti 3, siku ambayo hayati kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh alitoa wito wa kutangazwa "Siku ya Kimataifa ya Gaza".

Siku tatu kabla ya kuuwawa na Israeli wakati wa ziara yake katika mji mkuu wa Iran wa Tehran, Haniyeh alitoa wito kwa mataifa yote ya Kiarabu, Kiislamu na dunia nzima kujitokeza mitaani kuonesha mshikamano na watu wa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israeli na mateka wa Kipalestina katika magereza ya Israeli.

Kufuatia kifo chake, wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina walichukua jukumu la kuishi "wosia wa mwisho” na kuandaa maandamano dunia nzima.

Washiriki kutoka sehemu mbalimbali walikutana kwenye Uwanja wa Ayasofya siku ya Jumamosi, wakiandamana kupitia Eminonu, Hifadhi ya Gulhane, na mitaa inayozunguka Kucukayasofya. Mkusanyiko uliongezeka zaidi kwenye maeneo ya karibu.

Umati huo uliongezeka maradufu katika maeneo ya karibu./Picha:AA

Waandamanaji walibeba bendera za Uturuki na Palestina, wakiimba nyimbo za kudai uhuru wa Palestina.

Umati huo ulionesha upinzani mkali dhidi ya Israeli huku wakiiunga mkono Gaza kwa nyimbo kama vile "Palestina Huru kutoka mtoni hadi baharini," "Muuaji Marekani atoke Palestina," "Muuaji Israeli atoke Palestina," "Damu zetu na zivuje kwa ajili ya Al-Aqsa," na "Salamu Hamas, endeleza upinzani."

Mabango yenye ujumbe tofauti katika lugha za Kituruki, Kiarabu na Kiingereza zilizosomeka "Kuna mauaji ya Kimbari Gaza" "Israeli isitishe mauaji ya kimbari ," na "Mauaji yasitishwe watoto wasiendelee kufa."

Mabango yenye ujumbe tofauti katika lugha za Kituruki, Kiarabu na Kiingereza zilizosomeka "Kuna mauaji ya Kimbari Gaza" "Israeli isitishe mauaji ya kimbari ," na "Mauaji yasitishwe watoto wasiendelee kufa."/Picha: AA

Taasisi mbalimbali zikiwemo za The Free Jerusalem Platform na ile ya Prophet Loved Ones Foundation ziliandaa maandamano hayo kutoka uwanja wa Beyazıt hadi bustani ya Ayasofya. Picha za Haniyeh zilitawala maandamano hayo.

Baadaye, makundi hayo yakaunganika katika bustani ya Ayasofya, katika onesho la kuvutia la mshikamano.

Waandamanaji walipeperusha bendera za Uturuki na Palestina wakiimba nyimbo za kuunga mkono uhuru wa Palestina./Picha:AA

Israeli, ikikiuka azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano, imekabiliwa na shutuma za kimataifa kutokana na kuendelea na mashambulizi ya kikatili dhidi ya Gaza tangu shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na Hamas.

Tangu wakati huo, zaidi ya Wapalestina 39,500 wameuawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na karibu 91,300 kujeruhiwa, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.

Takriban miezi 10 baada ya vita vya Israeli, maeneo makubwa ya Gaza yapo kwenye magofu huku kukiwa na kizuizi cha chakula, maji safi na dawa.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo iliiamuru kusitisha mara moja mashambulizi yake katika mji wa kusini wa Rafah, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni 1 walikuwa wametafuta hifadhi kutokana na vita kabla ya kuvamiwa Mei 6.

TRT Afrika