Kongamano la NEXT: Hafla ya TRT World inayoleta vijana pamoja kuangazia  changamoto za kimataifa

Kongamano la NEXT: Hafla ya TRT World inayoleta vijana pamoja kuangazia  changamoto za kimataifa

Hafla hii maalum ya vijana ilizinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo 2022, ikiwajumuisha viongozi wa sekta tofauti pamoja na washawishi
Tukio la siku nzima la majadiliano linalenga kuleta pamoja watu wengi kutoka Uturuki na nchi nyingine. / Picha: TRT World

TRT World, imezindua duru ya pili ya kongamano la NEXT, tukio la kipekee la vijana linalolenga kujadili changamoto za dharura za kimataifa na kukuza ubadilishanaji wa mawazo.

Imepangwa kufanyika 20 Juni. Itakuwa hafla ya siku nzima, ya ana kwa ana, itakayoleta pamoja waandishi wa habari chipukizi, wasomi, wanachama wa mashirika yasiyo ya kiserikali, na wajasiriamali ambao wametoa michango muhimu katika nyanja zao.

Itafanyika katika Kituo cha maonyesho ya sanaa cha Zorlu mjini Istanbul (Zorlu PSM).

Mwaka huu, kauli mbiu mpya zitajadiliwa ili kutafuta majibu ya kisasa kwa maswali ya dharura kuhusu vyombo vya habari, teknolojia, sayari, biashara, uongozi, michezo, elimu, usafiri na mengineo. Kama sehemu ya hafla hiyo, masuala muhimu ya kijamii, kitamaduni na teknolojia yatakayoathiri pakubwa sana siku zijazo yatajadiliwa katika makundi na hotuba za ufunguzi.

Jukwaa lenye nguvu

NEXT inalenga kuwa jukwaa madhubuti la viongozi vijana, wanahabari, wasomi, wanachama wa mashirika ya kiraia, na wajasiriamali ili kueleza maono yao ya siku zijazo na kutoa suluhisho zinazohamasisha katika ulimwengu wa upamoja.

Mwaka jana, hafla hiyo ilifanikiwa kufanya mkusanyiko tofauti wa vijana zaidi ya 1,000 kutoka Uturuki na mataifa ya nje.

Walijihusisha katika mijadala ya kusisimua juu ya mada mbalimbali, ikijumuisha mada za kuvutia kama vile utalii wa anga za juu, miundo endelevu ya biashara na teknolojia ya kisasa.

Kando na mijadala ya kuvutia, eneo la ukumbi litaonyesha uzoefu wa akili bandia na uhalisia pepe, kutoa fursa za mazungumzo shirikishi na wageni maalum.

Sehemu maalum ya mitandao ya kijamii itaandaliwa na kutatengwa maeneo ya warsha kwa washiriki kujifunza kikamilifu.

Mwaka jana, hafla hiyo ilifanikiwa kuandaa mkusanyiko wa zaidi ya vijana 1000 tofauti, kutoka Uturuki na nje ya nchi.

Walijihusisha katika majadiliano changamfu juu ya mada mbali mbali za kuvutia kama vile utalii wa anga za juu, miundo endelevu ya biashara, warsha za NFT za kina, na teknolojia ya kisasa.

Hafla hiyo itawakaribisha wazungumzaji wengi kutoka Uturuki na nje ya nchi, akiwemo mpishi maarufu mtandaoni wa Kituruki Burak Ozdemir, anayejulikana pia kama CZN Burak.

Mjadala wake wenye mada ya , 'Ushirikiano Wenye Maana: Kupunguza Athari za Maafa Pamoja', utaangazia mitetemeko mikubwa ya ardhi ya hivi majuzi Uturuki iliyowaua zaidi ya watu 45,000.

Timu ya Ozdemir ilisafirisha vifaa katika maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa nchini, ikiwa ni pamoja na Hatay, mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na tetemeko la ardhi.

Kukabiliana na ubaguzi

Asma Elbadawi, ambaye alizaliwa nchini Sudan na kukulia nchini Uingereza na pia ni mchezaji wa mpira wa vikapu na kocha, pia atahudhuria hafla hiyo.

Elbadawi, ambaye pia ni mshairi , amekumbana na kupinga dhana potofu za kibaguzi katika maisha yake, haswa akichangia katika kampeni iliyofaulu kubatilisha marufuku ya hijab katika mpira wa vikapu wa kulipwa mnamo 2014.

Kongamano hilo pia litaandaa mazungumzo ya kipekee yanayotarajiwa na nyota wa zamani wa kandanda Frederic Oumar Kanoute.

Katika hafla ya uzinduzi wa mwaka jana, NEXT iliangazia vikundi 11 vya majadilio, warsha 7, wazungumzaji wakuu 26, na kuvutia zaidi ya washiriki 1000.

Kati ya zaidi ya maombi 2000 yaliyowasilishwa, takriban 1400 yalitokwa kwa Waturuki huku mengine yakitoka nchi zingine .

Wageni wa tabaka mbalimbali wa kimataifa walishiriki katika kongamano hilo , wakiwakilisha nchi mbalimbali pamoja na Marekani, Kanada, Uingereza, Italia, Uholanzi, Sudan, Chile, Pakistan, India, Jordan, Namibia, Tanzania na Nigeria.

Usajili wa kongamano hilo unaweza kufanywa hapa: https://next.trtworldforum.com/.

TRT Afrika